Nembo ya Dominika ya Neno la Mungu. Nembo ya Dominika ya Neno la Mungu. 

Tarehe 21 Januari 2024 ni Dominika ya V ya Neno la Mungu

Taarifa kutoka Baraza la Kipapa la Uinjilishaji,Dominika tarehe 21 Januari 2024 itaadhimishwa Dominika ya V ya Neno la Mungu.Ibada itaongozwa na Baba Mtakatifu ambapo kutakuwa na fursa ya kuwathibitisha wahudumu 2 wa masomo ya Neno na 9 wa huduma ya Makatekista.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Dominika ya tano ya Neno la Mungu itaadhimishwa tarehe 21 Januari 2024, siku iliyoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 30 Septemba 2019. Kauli mbiu ya toleo hili iliyotolewa katika Injili ya Yohane inasema: “Kaeni katika Neno langu” (Yh 8:31).  Kwa njia hiyo saa 3,30 asubuhi, Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuongoza  maadhimisho ya Ekaristi Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na katika muktadha huo, kwa lengo la kufufua dhamana waliyonayo waamini katika maarifa ya Maandiko Matakatifu watakao kuwapo watapewa zawadi ya Injili ya Mtakatifu Marko.

Kupewa neno la Mungu mikononi katika siku ya Neno la Mungu
Kupewa neno la Mungu mikononi katika siku ya Neno la Mungu

Kwa mujibu wa taarifa la Baraza la Kipapa la Uinjilishaji kitengo cha masuala msiingi ya uinjilishaji limebainisha kuwa "Wakati wa maadhimisho, hayo kutakuwa na fursa ya kuwathibitisha wahudumu wa masomo na huduma Katekista kwa walei wanawake na wanaume, hasa watu 2 watapokea huduma ya kusoma masomo na 9 kwa huduma ya Katekista." Ni waamini walei wanaoazimia kuwawakilisha Watu wa Mungu na wanatoka nchin: Brazil, Bolivia, Korea, Chad, Ujerumani na Antilles. Tukio hilo litaoneshwa moja kwa moja (Mbashara kwenye runinga na Vyombo vya Habari vya Vatican na utiririshaji kwenye tovuti ya Habari za Vatican (vaticannews.va) na moja kwa moja na vituo vikuu vya televisheni ulimwenguni, Nchini Italia, ni miongoni mwake kwa Televisheni ya Rai 1.

Papa atawathibitisha huduma ya makatekista
Papa atawathibitisha huduma ya makatekista

Kutoka kitengo cha masuala Msingi ya Uinjilishaji katika Ulimwengu wa Baraza la kipapa la  Uinjilishaji, iliyoteuliwa na Baba Mtakatifu kuendeleza tukio hilo, imewezeza kutoa msaada wa bure wa masomo ya kiliturujia na kichungaji kupatikana mtandaoni kuwa muhimu kwa ajili ya maisha Neno la Mungu na maombi katika jumuiya, familia na mtu binafsi. Maandishi, yanayopatikana mwaka huu katika toleo la dijitali pekee, yanaweza kupakuliwa mtandaoni katika  lugha ya:Kiitaliano, Kiingereza, Kihispania, Kireno, Kifaransa, Kipolandi, katika  tovuti ya:www.evangelizatio.va.

Hawa ni wahudumu wa kusoma neno na makatekista 2022
Hawa ni wahudumu wa kusoma neno na makatekista 2022

Ni chombo kinachotoa mapendekezo ya kuhimiza kukutana kwa kina na Neno la Mungu katika jamii, katika familia, katika maisha ya kila siku, na pia inajumuisha makala, tafakari, maandiko ya kuabudu na mapendekezo ya kichungaji. Katika maadhimisho ya Jumapili ya Neno, Baba Mtakatifu anatarajiwa kuzindua rasmi Mwaka wa Sala, kwa ajili ya maandalizi ya Jubilei ya 2025. Baada ya kuhimiza tafakari ya nyaraka na utafiti wa matunda ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatikano mwaka 2023, kwa wosia wa Baba Mtakatifu Francisko, 2024 itawekwa wakfu, katika majimbo ya dunia, kwa ajili ya kugundua upya umuhimu wa sala.

Dominika V ya Neno la Mungu, Papa ataongoza ibada ya misa takatifu 21 Januari 2024
15 January 2024, 15:50