Papa amemteua Padre Thomas Obiatuegwu kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Orlu,Nigeria
Vatican news.
Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 5 Januari 2024 amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Orlu (Nigeria), Mheshimia Padre Thomas Ifeanyichukwu Obiatuegwu, wa jimbo la Orlu, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Joseph huko Umuna, kwa kupewa makao yake huko Orreacelia.
Wasifu wake
Padre Thomas Ifeanyichukwu Obiatuegwu alizaliwa tarehe 1 Januari 1966 huko Uli, Jimbo la Anambra. Alijiunga na Seminari Ndogo huko Umuowa, Seminari Kuu ya Mtakatifu Joseph huko Ikot-Ekpene(1987-1991), na baadaye Seminari ya Ukumbusho ya Bigard huko Enugu(1991-1995). Alipata Shahada ya Uzamili katika Falsafa Chuo Kikuu cha Navarra, Pamplona, Hispania(2001-2003) na Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Umma na Sera kutoka Chuo Kikuu cha Indiana nchini Marekani(2005-2008).
Tarehe 26 Agosti 1995 alipewa daraja la Upadre kwa ajili ya Jimbo la Orlu. Alishikilia nyadhifa nyingine kama vile: Kuongoza Kikanisa cha hospitali ya Amaigbo (1995-1997); Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Theresa huko Amauju, Isunjaba(1997-2001); Padre wa Parokia ya Mtakatifu Patrick huko Kokomo, Indiana, Marekani(2004-2010); Padre a Kikanisa cha Jeshi la Marekani(2010-2017); Padre wa parokia ya Rozari Takatifu huko Orlu(2017-2018); paroko wa Mtakatifu Mikaeli huko Urualla(2018-2023); Mkuu wa eneo la kichungaji la Mtakatifu Mikaeli (2018-2023); tangu 2023 Paroko wa Mtakatifu Yosefu huko Umuna, Orlu.