Askofu MkuuPaglia kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Ulimwenguni(WMA),Chama cha Madaktari cha Marekani(AMA)wanafanya kongamano 18/19 Januari 2024 mjini Vatican. Askofu MkuuPaglia kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Ulimwenguni(WMA),Chama cha Madaktari cha Marekani(AMA)wanafanya kongamano 18/19 Januari 2024 mjini Vatican. 

WMA,AMA na PAV mjini Vatican kwa kongamano la Ushirikiano wa Kimataifa wa Utafiti wa Matibabu kimaadili

Ni Januari 18-19,2024 kuhusu Marekebisho ya Tamko la Helsink,lililoandaliwa na Chama cha Madaktari Ulimwenguni(WMA),Chama cha Madaktari wa Marekani(AMA) na Chuo cha Kipapa cha Maisha,(PAV).Kongamano linalenga masuala ya masharti ya kuhakikisha uadilifu na uaminifu wa utafiti katika nchi maskini.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Chama cha Madaktari Ulimwenguni (WMA) kwa ushirikiano na Chama cha Madaktari cha Marekani (AMA) na Chuo cha Kipapa cha Maisha, (PAV)wameandaa Kongamano la Marekebisho ya Tamko la Helsinki. Tukio hilo muhimu, litakalofanyika tarehe 18-19 Januari 2024 katika Ukumbi wa Sinodi ya zamani mjini Vatican, litaakisi utafiti wa matibabu na majaribio katika mazingira duni ya rasilimali. Azimio la Helsinki, lililoandaliwa hapo awali mnamo 1964 na Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Madaktari Ulimwenguni, hutumika kama mwongozo wa kimaadili wa majaribio ya mwanadamu katika taaluma ya matibabu. Mnamo 2022, kwa kutambua mazingira yanayoendelea ya huduma ya afya, chama cha Madaktari Ulimwenguni(WMA) kiliteua kikundi kazi kuanza mchakato wa marekebisho. Ili kuhakikisha mtazamo tofauti na wa kimataifa,(WMA)kilianzisha mfululizo wa makongamano ya kikanda, huku mkutano ujao wa Vatican ukiwa ni hatua muhimu.

Dk. Lujain AlQodmani, Rais wa Chama cha WMA, alisisitiza dhamira ya kuendeleza huduma za afya duniani, hasa katika maeneo ambayo watu walio hatarini wameathirika zaidi. “Uchunguzi muhimu wa utafiti wa kimatibabu katika mazingira yenye rasilimali duni unalingana na dhamira ya WMA ya kuhakikisha mwenendo wa kimaadili na uwajibikaji wa utafiti wa kimatibabu duniani kote," alisisitiza Dk. AlQodmani. Naye Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, alisisitiza "kwamba ushirikiano kati ya Chuo hicho PAV na  Chama cha Madkatari Ulimwenguni WMA tayari umeoneshwa katika siku za nyuma, na mkutano wa 2017 kuhusu masuala ya mwisho wa maisha na hivi karibuni kuhusu suala la chanjo katika muktadha wa  janga la Uviko19. Ushirikiano kati ya taasisi zetu, katika hafla ya kuadhimisha miaka 60 ya Azimio la Helsinki, ni ishara muhimu ya mazungumzo na kutafuta maadili ya pamoja, katika ulimwengu ambao umegawanyika sana leo”.

Naye Monsinyo Renzo Pegoraro, Kansela wa Chuo cha Kipapa cha maisha (PAV,) aliakisi changamoto za mada ya mkutano huo, katika maadhimisho ya miaka 60 ya Azimio la Helsinki, kuleta changamoto za kimaadili katika utafiti wa matibabu unaohusisha wanadamu. "Tunahitaji kujiuliza jinsi ya kufanya matokeo kupatikana kwa idadi ya watu katika nchi maskini wa rasilimali wakati tukiendelea kuwapa fursa ya kupata teknolojia na dawa. Mtazamo ni kukuza ushirikiano wa kweli katika kiwango cha kimataifa ili kushiriki vyema mizigo na matokeo ya utafiti. PAV inajisikia kujitolea kwa ari hii chanya na yenye kujenga na WMA, kwa ajili ya kufufua na iwezekanavyo marekebisho ya Azimio la Helsinki ambalo linatilia maanani mtazamo huu", aliongeza Bi. Pegoraro.

Dk. Jung Yul Park, Mwenyekiti wa Baraza la Madaktari Ulimwenguni (WMA) alisisitiza mwelekeo wa mkutano huo katika kutatua changamoto za kimaadili za kufanya tafiti za matibabu katika mazingira yenye rasilimali chache. "Lazima tusawazishe kutafuta maarifa ya kisayansi na jukumu la kimaadili la kulinda ustawi wa washiriki," alisema Dk. Park. Alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya matibabu unaendelea kwa washiriki wa utafiti baada ya kumalizika kwa tafiti.

Kongamano hilo linalenga kushughulikia masuala ya kimsingi kama vile masharti ya awali ya kuhakikisha uadilifu na uaminifu wa utafiti katika nchi maskini wa rasilimali na njia za kufanya matokeo ya utafiti kupatikana kwa watu hao. Ushirikiano kati ya Chama cha Madaktari Ulimwenguni (WMA), Chama cha Madaktari cha Marekani (AMA) na Chuo cha Kipapa cha Maisha,(PAV) unalenga kukuza ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya marekebisho ya maana ya Azimio la Helsinki, kuakisi changamoto na mahitaji ya jumuiya mbalimbali za kimataifa. Kwa habari zaidi kuhusu mkutano huo, ukijumuisha programu na maelezo, tafadhali tembelea Mkutano wa WMA wa Marekebisho ya Tamko la Helsinki.

https://www.wma.net/news-post/global-collaboration-for-ethical-medical-research-wma-ama-and-pav-unite-in-vatican-city/

Chama cha Madaktari Ulimwenguni (WMA),Chama cha Madaktari cha Marekani (AMA) na Chuo cha Kipapa cha Maisha,(PAV)
15 January 2024, 16:13