Vyuo Vikuu vya Kipapa vyatoa kozi ya mtandaoni juu ya Ikolojia Fungamani
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Vyuo vikuu vya Kipapa(vinavyoendeshwa na Kanisa) mjini Roma vitakutana pamoja ili kuzindua Diploma mpya ya Pamoja ya Ikolojia Fungamani. Hili ni wazo kuu la Papa Francisko, linalosisitiza muunganiko wa masuala ya mazingira, kiuchumi, kisiasa, kijamii na kimaadili. Kozi hiyo inaanza mwezi huu Januari hadi Juni 2024, na kufundishwa na kundi la kimataifa la wasomi, viongozi na wanaharakati mashuhuri.
Sayari inakaribia kuvunjika
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Vatican, Vyuo Vikuu vya Kipapa vimebainisha kwamba kozi hiyo ni jibu la "changamoto isiyo na kifani inayoikabili sayari. Mwaka 2015, Papa Francisko alituzawadia Laudato si',(Laudato si’)waraka wake wa kihistoria unaowaalika watu wote wenye mapenzi mema kuchukua hatua juu ya mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo, wanavyosema, kama vile Papa Francisko anavyotambua katika Waraka wake wa hivi karibuni wa Laudate Deum,(Laudate Deum,)majibu yetu hayajatosheleza, na ulimwengu tunamoishi unaporomoka na huenda unakaribia kuvunjika.
Maelezo ya kozi hiyo
Diploma ya Pamoja ilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016, lakini sasa inatolewa kwa mara ya kwanza kwa lugha ya Kiingereza. Kozi hiyo itakuwa na vingele sita vya dakika 90 kila kimoja, vinafanyika kuanzia Januari hadi Juni 2024, kila Alhamisi ya tatu ya mwezi kuanzia saa 7.30 hadi 9.00 alasiri masaa ya Roma. Pia kutakuwa na warsha mnamo mwezi Machi na mkutano wa kimataifa kwa njia ya mtandao kuhusu Laudate Deum mnamo mwezi Mei 2024.
Kozi inazindiliwa 25 Januari 2024
Kozi hiyo itazinduliwa rasmi tarehe 25 Januari 2024, lakini usajili utabaki wazi hadi tarehe 31 Machi 2024. Kwa maelezo zaidi, yakijumuisha kiungo cha kujiandikisha katika kozi bonyeza hapa:(can be found here. )