2024.01.04: Watawa wa kibenedikitini kutoka Argentina wamefika kuishi katika monasteri ya Mater Ecclesiae. 2024.01.04: Watawa wa kibenedikitini kutoka Argentina wamefika kuishi katika monasteri ya Mater Ecclesiae. 

Watawa wa Vatican,Wabenediktini kutoka Argentina wamewasili Mater Ecclesiae

Watawa sita wa Shirika la Wabenediktini wa Abasia ya Mtakatifu Scholastica wa Victoria,wakiwa wamesindikizwa na Mkuu wao waliwasili tarehe 3 anuari 2024,mjini Roma. Walikaribishwa na Kardinali Vérgez,Gavana wa Mji wa Vatican.Wataunda jumuiya ya watawa katika monasteri ambayo ilikuwa nyumba ya Papa Benedikto XVI kwa karibu muongo mmoja tangu alipojiuzulu hadi kifo chake.

Vatican News

Watawa Wabenediktini kutoka Argentina ambao Papa Francisko aliwaalika kuishi katika  Monasteri ya Mater Ecclesiae, iliyoko katikati ya bustani ya Vatican ambayo kwa karibu muongo mmoja ilikuwa makazi ya Papa Mstaafu, Benedikto XVI, baada ya kujiuzulu kwake kihistoria, waliwasili asubuhi,ya tarehe 3 Januari 2024.  Ni watawa sita wa Shirika la Wabenediktini wa Abasia ya Mtakatifu  Scholastica wa Victoria, katika Wilaya ya  Buenos Aires (Jimbo la Isidro,) nchini Argentina. Papa Francisko alikuwa amewaalika kwa barua iliyoandikwa kwa mkono wake   tarehe 1 Oktoba 2023 na watawa  hao walikubali mwaliko huo kwa ukarimu.

Watawa wakikaribishwa na Kardinali Vérgez

Gavana wa Mjini wa Vatican, Kardinali Fernando Vérgez Alzaga, ndiye aliyekwenda Uwanja wa ndege wa Fiumicino alfajiri kuwapokea na, aliwakaribisha watawa hao mara baada ya kuwasili mjini Roma. Kama ilivyoanzishwa na Papa, Gavana  huyo atawajibika kwa masuala yote yanayohusu Monasteri ya Mater Ecclesiae. Watawa hawa 6 walisindikizwa mjini Vatican  na Mkuu wa Shirika la Monasteri ya Mtakatifu Scolastina wa Victoria na mtawa mwingine kumsaidia katika safari. Mara tu walipofika Mater Ecclesiae, watawa wote 6 walikwenda katika Groto ya  Lourdes iliyoko katika  bustani ya Vatican kwa wimbo na sala mbele ya sanamu ya Mama Maria wa Lourdes ambayo ni nakala inayofanana na sanamu inayoheshimiwa huko Massabielle, Nchini Ufaransa.

Watawa wa Kibenediktini ambao wanaishi katika Monasteri ya Mater Ecclesiae
Watawa wa Kibenediktini ambao wanaishi katika Monasteri ya Mater Ecclesiae

Maono ya Mtakatifu Yohane Paulo II

Tangu tarehe 3 Januari 2024  Mater Ecclesiae, ambayo haijawahi kukoma kuwa mahali pa sala, kwa hiyo imerejea kuwa makao ya Shirika la  kutafakari, kama alivyotaka  Mtakatifu Yohane Paulo II, ambaye kwa muda mfupi wa  Maisha ya Tafakari ya tarehe 25 Machi 1994 aliidhinisha  kwa kisheria katika mji wa Vatican uwepo wa  Monasteri ya Watawa wa ndani, kwa kusali ili “kumsaidia Baba Mtakatifu katika mahangaiko yake ya kila siku kwa Kanisa zima, kwa huduma ya sala, kuabudu, sifa na malipizi, hivyo kuwa ni uwepo wa kusali katika ukimya na upweke.” Mtakatifu Yohane Paulo II alilipatia Jina la Nyumba hiyo Mater Ecclesiae, yaani ‘ Mama wa Kanisa’. Kulingana na sheria ya monasteri, utabiri ulikuwa ni kila baada ya  miaka mitano kubadilisha watawa wa kimonasteri. Watawa wa mwisho walikuwa huko hadi Novemba 2012, na baadaye wakaanza kazi ya kuikarabati.

Nyumba ya Papa Benedikto XVI

Kufuatia na kujiuzulu kwake kutoka Upapa, mnamo tarehe 11 Februari 2013,  Papa Benedikto XVI alionesha nia yake ya kuishi  katika nyumba ya Mater Ecclesiae. Baada ya kukaa kwa muda mfupi katika Jumba la Kitume huko Castel Gandolfo, Papa Mstaafu kisha tarehe 2 Mei 2013 alihamia katika Monasteri, ambako aliishi ndani humo huku akijishughulisha kati ya kujisomea, muziki na sala hadi kifo chake  kilichomjia tarehe 31 Desemba 2022.

Watawa wa Kibenediktini ambao wameanza kuishi Mater Ecclesiae tangu 3 Januari 2024
Watawa wa Kibenediktini ambao wameanza kuishi Mater Ecclesiae tangu 3 Januari 2024

Pamoja naye walikuwa Memores Domini, yaani walei wanawake waliowekwa wakfu  4 wa Harakati ya Comunione e Liberazione, yaani Umoja na Ukombozi  ambao walimsaidia hadi kufa kwake na katibu wake  kibinafsi Askofu Mkuu Georg Gänswein, ambaye aliendelea kuishi katika Monasteri hadi uhamisho wake wa kurudi katika  jimbo lake asili la Freiburg, nchini Ujerumani, mnamo tarehe 1 Julai 2022. Na hivi karibuni Baba Mtakatifu Francisko alikutana na Askofu Mkuu Gänswein na Memores yaani wali  wote waliokuwa wanaishi na Papa Benedikto XVI katika mkutano wa  faragha kwenye  Jumba la Kitume.

Papa Francisko awasalimia

Kwa dakika chache baada ya kuhitimisha Misa Takatifu, iliyoongozwa na Papa Francisko tarehe 6 Januari 2024 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, taarifa kutoka vyombo vya habari Vatican ilibanishwa kuwa kabla ya Maadhimisho ya Misa Takatifu, Baba Mtakatifu alisalimia kikundi cha wamonaki wa Kibenedikini kutoka nchini Argentina ambao wamefika hivi karibuni kuishi katika Monosteri ya Mater Ecclesiae.

Watawa wakibenediktini
Watawa wakibenediktini
Watawa wa kibenediktini kufika Monasteri ya Mater Ecclesiae mjini Vatican
08 January 2024, 11:51