Tafuta

Nyumba zilizoharibiwa kusini mwa Gaza Nyumba zilizoharibiwa kusini mwa Gaza  (ANSA) Tahariri

Acha mauaji

Tunachapisha Tahariri ya mwariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk.Andrea Tornielli kuhusu maneno ya Katibu wa Vatican,Kardinali Pietro Parolin, juu ya vifo vya watu 30m000 huko Gaza.

Andrea Torinielli

Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, mara baada ya mauaji yaliyofanywa na magaidi wa Hamas mnamo tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya familia zenye amani za Israel alifafanua shambulio hilo kama la “kinyama.” Alikuwa ametaja kuachiliwa kwa mateka hao kama kipaumbele, pia akizungumzia haki ya Israel ya kujilinda na kuonesha kigezo kama mkutano wa kila mwaka wa kuadhimisha Makubaliano ya Lateran, kati ya Italia na Vatican, Kardinali Parolin, akizungumza na waandishi wa habari, alitumia maneno yasiyo na shaka juu ya kile kinachotokea Gaza.

Kwa upande wake alisema “lawama za wazi na zisizo na kikomo za kila aina ya chuki dhidi ya Wayahudi”, lakini wakati huo huo alisisitiza “ombi kwamba haki ya ulinzi wa Israel ambayo ilitolewa ili kuhalalisha operesheni hii iwe sawa na kwa hakika na vifo elfu 30 ambayo siyo.” Kadinali huyo aliongeza: “Nadhani sote tumekasirishwa na kile kinachotokea na mauaji haya, lakini lazima tuwe na ujasiri wa kusonga mbele na sio kupoteza matumaini.” Mwaliko wa kutoshindwa na kukatishwa tamaa, kwa kudhaniwa kuwa ni kutoepukika kwa msururu wa vurugu ambao hauwezi kamwe kuwa kielelezo cha amani, lakini kwa bahati mbaya unahatarisha kuzalisha chuki mpya.

Akihojiwa na Gazeti la matukio  ya kila siku(Fatto quotidiano),mwandishi na mshairi Edith Bruck - ambaye katika majira ya kuchipua, mnamo ya 1944, akiwa na umri wa miaka kumi na tatu, alitekwa katika geto la Hungaria la Sátoraljaújhely na kuhamishwa hadi Auschwitz - pia alionesha misimamo kama hiyo. Alielekeza ukosoaji mkali dhidi ya Waziri Mkuu wa sasa wa Israel, huku akisema kwamba “ameharibu Wayahudi wa diaspora kwa sababu ameimarisha tena chuki dhidi ya Wayahudi ambayo haijawahi kutoweka na sasa imeongezeka.” Bruck aliongeza imani yake kwamba kwa sera hii magaidi hawataondolewa kamwe. Mawazo ya Kardinali na mshairi wa Kiyahudi ni maneno yanayotolewa na mtazamo wa uhalisia katika janga linaloendelea. Kwa upande wa Vatican chaguo la upande daima ni la waathriwa. Na kwa hivyo kwa Waisrael waliouawa nyumbani katika kibbutz walipokuwa wakijiandaa kusherehekea siku ya Simchat Torah, kwa ajili ya mateka walioondolewa kutoka katika familia zao, na kwa raia wasio na hatia - theluthi moja yao watoto - waliouawa na mabomu huko Gaza.

Hakuna mtu anayeweza kufafanua kinachotokea katika Ukanda huo kama“uharibifu wa dhamana” katika mapambano dhidi ya ugaidi. Haki ya kujitetea, haki ya Israel kuwafikisha wale waliohusika na mauaji ya Oktoba mbele ya sheria, hayawezi kuhalalisha mauaji haya. Katika sala ya Malaika Bwana mnamo tarehe 17 Desemba iliyopita, baada ya kuuawa kwa wanawake wawili wa Kikristo ambao walikuwa wamekimbilia katika parokia ya Gaza, Papa Francisko alisema: “Raia wasio na silaha wanakabiliwa na milipuko ya mabomu na risasi ... Wengine wanasema: “Ni ugaidi, ni vita.” Ndiyo, ni vita, ni ugaidi. Hii ndiyo sababu Maandiko yanasema kwamba: “Mungu anakomesha vita... anavunja pinde na kuvunja mikuki” (taz. Zab 46:9). Na tuombe kwa Bwana amani.” Mwanzoni mwa Kwaresima, wakati sehemu  kubwa ya waathiriwa wasio na hatia ikiendelea, wito huu unazidi kusisitiza, kwa kuomba silaha zinyamazishwe kabla haijachelewa kwa ulimwengu wetu ukingoni mwa shimo.

14 February 2024, 17:11