2024.01.31 Askofu Mkuu Rino Fisichella alikuwa Brazil kuzungumza juu ya Jubilei ya 2025 2024.01.31 Askofu Mkuu Rino Fisichella alikuwa Brazil kuzungumza juu ya Jubilei ya 2025 

Ask.Mkuu Fisichella:Jubilei ya 2025 ni fursa nzuri ya kichungaji

Msaidizi wa Mwenyekiti wa Baraza la Uinjilishaji alikuwa mjini Brasilia kwa ajili ya mkutano wa kitaifa wa ‘Preparando o Jubileu da Esperanca,’ulioandaliwa tarehe 29 na 30 Januari 2024 na Baraza la Maaskofu wa Brazil,ambapo alizungumza juu ya matumaini katika ulimwengu wa kisasa na kuelezea mipango kwa jumla ya Mwaka Mtakatifu.

Na angella Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu  Rino Fisichella, Mwenyekiti Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Unjilishaji alitoa hotuba yake katika mkutano wa kitaifa wenye kauli mbiu “Preparando o Jubileu da Esperanca” yaani kuandaa Jubilei kwa matumaini ulioandaliwa tarehe 29 na 30 Januari 2024  na Baraza la Maaskofu wa Brazil, katika Nyumba ya Luciano, huko mjini Brasilia na kusimamiwa na kikundi cha uhamasishaji wa Jubilei, timu iliyoundwa na maaskofu ili kusaidia maandalizi ya mwaka mtakatifu wa Jubilei katika makanisa nchini Brazil.

Askofu Mkuu Fischella akiwa anahutubia huko nchini Brazil
Askofu Mkuu Fischella akiwa anahutubia huko nchini Brazil

Zaidi ya wajumbe mia tatu walifika kutoka majimbo mbalimbali ya Brazil, wakiwemo maaskofu, watu wa Mungu walei,  wawakilishi wa harakati na mashirika; Pia alikuwepo Balozi wa Vatican  Askofu Mkuu  Giambattista Diquattro, ambaye katika siku ya kwanza ya kazi, alijikita katika mada ya: “Mtazamo wa hatua ya uinjilishaji ya Baraza la Maaskofu Brazil CNBB), kuhusu ‘Changamoto za utendaji wa uinjilishaji wa Kanisa nchini Brazili’, kwenye Jubilei. Katika Maandiko Matakatifu na mada iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa uteuzi wa mwaka 2025, alisisitiza jinsi ambavyo “Kanisa la Brazil linavyothibitishwa katika ari ya matarajio, shauku na hamasa katika kuifuata njia pekee ambayo ni Kristo Yesu”.

Askofu Mkuu akuhutubia Mkutano kwa wahusika wa katekesi huko Brazil
Askofu Mkuu akuhutubia Mkutano kwa wahusika wa katekesi huko Brazil

Katika hotuba yake Askofu Mkuu Fisichella alieleza kwamba, Jubilei ya Kawaida ya 2025 ni sehemu ya mapokeo ya  tangu mwaka 1300 na kwamba  Kanisa la Roma limejipanga hasa kuwakaribisha mahujaji wengi watakaofika katika mji wa Petro na Paulo kuvuka Mlango Mtakatifu na kwamba Mwaka wa Neema kwanza kabisa ni uzoefu wa imani unaomruhusu mtu kuishi huruma ya Baba kwa utimilifu, pamoja na pendekezo la kichungaji lisilopaswa kudharauliwa na kwa hivyo mada ya matumaini inapaswa kuzingatiwa maudhui ya upendeleo ya uinjilishaji.

Na hasa alipozungumza juu ya tumaini, Askofu Mkuu Fisichella aliwasihii waamini kueleleza mtazamo wao kwa maana tofauti ambayo sio tu kwa sasa na mara moja tu, bali wenye uwezo wa kuwekwa ndani hali ya kusubiriwa kwa uangalifu unaostahili, akionesha kwamba mawazo ya kisayansi badala yake yamepunguza kwa kiasi kikubwa haja ya matumaini, na badala yake watu wetu wa kisasa wanahitaji matumaini. Kudumisha tumaini hai si utume tu ambao Wakristo walipokea kutoka kwa Bwana alipowatuma kutangaza Injili yake katika kila sehemu ya ulimwengu, lakini ni kwamba leo linakuwa jukumu kubwa zaidi kwa sababu katika upotovu ambao majaribio katika sekta mbalimbali za maisha ya kibinafsi na kijamii, ni jambo la dharura na la lazima kwa sauti za wale wanaoleta neno na ishara yenye uwezo wa kutazama sasa kwa macho tofauti.”

Askofu Mkuu Fischella akihutubia
Askofu Mkuu Fischella akihutubia

Kwa wawakilishi wa majimbo ya  Brazil, Askofu Mkuu  Fisichella alisema kwamba matumaini yanakuja kusaidia kuendeleza sasa kwa kuipatia maana inayohitaji na kwamba yanaambatana na chaguo ambazo kila mtu ameitwa kufanya kwa uwajibikaji. “Tunatumaini kutoa maana kwa sasa ambayo inaweka uchaguzi wa uhuru wa kujenga maisha ya kibinafsi juu ya ukweli wa mtu mwenyewe na ulimwengu”, alifafanua huku  akibainisha kuwa “tumaini hufanya safari ya maisha kuwa hija ya kweli, kwa sababu inasaidia kuondoa uchovu, kutokuelewana, uchungu... na inatia hisia ya furaha na utulivu ambayo hutokea kwa usahihi kutokana na uwezo wa kutazama sasa kama msingi wa kweli wa wakati ujao wa kweli wa uzima wa milele.”

Tarehe 30 Januari 2024, msimamizi wa Baraza la Uinjilishaji alionesha ratiba ya  jumla ya Mwaka wa Jubile na mbinu za ushiriki. “Tufikirie makundi yote yatakayokuwepo, kama vile vijana kwa mfano. Wacha tuwatie moyo kushiriki na kujiandaa. Utabiri ni kwamba tutakuwa na vijana milioni Moja na Nusu. Idadi kama hiyo pia inachukuliwa kwa matukio mengine, alihitimisha Askofu  Fisichella, akisisitiza kwamba ana imani kuwa Jubilee itakuwa hafla kubwa ya kichungaji.

 

01 February 2024, 18:37