Tafuta

Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina Balozi mpya wa Vatican nchini Japan. Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina Balozi mpya wa Vatican nchini Japan.  (Vatican Media)

Askofu Mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina Balozi wa Vatican Nchini Japan

Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina alizaliwa mwaka1965, nchini Venezuela. Tarehe 26 Agosti 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 13 Juni 1998 akajiunga na Utume wa Diplomasia ya Kanisa na kutumwa huko nchini: Sudan, Ghana, Malta, Nicaragua, Japan and Slovenia. Tarehe 21 Mei 2016 akateuliwa kuwa Balozi nchini Congo Brazzaville na Gabon na kupandishwa hadhi kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 28 Mei 2016. Sasa yupo Japan!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Japan. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Haiti, na amewahi kuwa pia Balozi wa Vatican nchini Congo Brazzaville na Gabon. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina alizaliwa tarehe 29 Januari 1965, Jimboni San Cristóbal de Venezuela nchini Venezuela. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 26 Agosti 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Japan
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Japan

Tarehe 13 Juni 1998 akajiunga na Utume wa Diplomasia ya Kanisa na kutumwa huko nchini: Sudan, Ghana, Malta, Nicaragua, Japan and Slovenia. Tarehe 21 Mei 2016 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Congo Brazzaville na Gabon na kupandishwa hadhi kuwa Askofu mkuu. Akawekwa wakfu tarehe 28 Mei 2016. Tarehe 4 Juni 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Haiti. Na ilipogota tarehe 25 Januari 2024, Baba Mtakatifu Francisko akamteua Askofu mkuu Francisco Gerardo Escalante Molina kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Japan.

Uteuzi Japan
02 February 2024, 13:35