Baraka ya Ubalozi mpya wa Vatican huko Myanmar
Vatican News
Ilikuwa tarehe 16 Desemba 2023, ambapo Makao ya Mwakilishi wa Kitume katika Ubalozi wa Vatican huko Yangon, Myanmar yalibarikiwa. Miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo ni Kardinali Charles Maung Bo, Askofu Mkuu wa Yangon. Askofu Noel Saw Naw Aye, askofu msaidizi wa Yangon na Monsinyo Andrea Ferrante, anayesimamia Mambo katika Ofisi ya Ubalozi. Baadhi ya wawakilishi wa kamati ya ‘Dini kwa ajili ya Amani Myanmar’ pia walikuwepo.
Baada ya hotuba ya utangulizi ya Ubalozi Mdogo, Kardinali Bo aliongoza sala ya baraka na kusoma ujumbe kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican. Baada ya hapo, aliwasalimia waliokuwepo, ambapo alionesha furaha yake na shukrani zake kwa ufunguzi wa Uwakilishi wa Papa nchini Myanmar, huku akisisitiza jinsi tukio hilo lilivyo ishara ya matumaini kwa nchi hiyo, hasa kwa kuzingatia hali ya ukosefu wa utulivu na ghasia inayoikabili.