Ukraine,Kard.Parolin:ni huzuni hakuna matarajio mengine ya mazungumzo!
Vatican News
Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiulizwa maswali na waandishi wa habari nje ya tukio la uzinduzi wa kituo kipya cha uchunguzi wa kimatibabu cha hospitali ya Magonjwa ya Ngozi ya Bikira Mkingiwa(IDI), jijini Roma jioni tarehe 26 Februari 2024 awali kuhusu maandamano ya Pisa na Firenze nchini Italia yaliyoshuhudia mapigano kati ya polisi na wanafunzi alisema :“Kila mtu anaitwa kuwa mwenye busara. Na kutumia mabango“hakika ni kushindwa” hata hivyo “inaweza kujidhihirisha kwa njia sahihi. Lazima kila wakati tutafute njia sahihi ya kuelezea mahitaji yetu, hata maandamano yetu na wakati huo huo tuwe tayari kuwakaribisha.”
Papa Francisko yuko vizuri
Kadinali Parolin pia alizungumza kuhusu afya ya Papa Francisko na kuthibitisha kwamba Papa yuko Mzima, Alikuwa na kipindi hiki cha mafua lakini akapona, ilikuwa inanibidi niende kwake jioni ya leo hii lakini niko hapa, kikao kilikuwa hakijasitishwa. Kwa hiyo ina maana kwamba amepona na kuendelea na shughuli zake za kawaida.”
Inasikitisha kwamba hakuna matarajio ya amani kwa Ukraine
Katika ngazi ya kimataifa zaidi, Katibu wa Vatican alibainisha kifo cha mpinzani wa Urussi Alexei Navalny, kwamba “ingekuwa muhimu kufafanua kile kilichotokea. Hii ingesaidia kuwahakikishia hata wale ambao kwa hakika wanatoa tafsiri fulani ya kifo hicho.” Lakini pia hali ya Ukraine, uwezekano wa mazungumzo ni katikati ya tahadhari ya Kardinali ambaye, akimaanisha ujumbe wa Kardinali Matteo Zuppi, rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI,) na kuwa “tunajaribu kufanya kazi ili kufanya utaratibu huu ambao ulianzishwa wakati wa ziara yake huko Kyiv na Moscow kwa ajili ya kurudi kwa watoto na vijana kwa Ukraine rahisi kidogo.” Kwa kuongezea Kardinali alisema “wakati huo kwamba hii inaweza kukuza njia za amani. Kwa sasa inaonekana kwangu kwamba kuna hili tu, kwamba hakuna matarajio mengine ya mazungumzo na hii inasikitisha sana.” Kuhusiana na maandamano ya wakulima, ambao walirudi Brussels kuomba hatua nzuri zaidi kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Kardinali Parolin alisisitiza kwamba tu kwa mazungumzo mazito na kusikiliza mahitaji yaliyotolewa na wakulima tunaweza kufikia matokeo, na kufikia mkutano.”
Mashambulio dhidi ya Wakristo nchini Burkina Faso ni ya kusikitisha
Hatimaye, Kardinali alilezea “hali ya hatari" nchini Burkina Faso, ambapo Wakristo kumi na watano waliuawa wakati wa ibada ya Dominika: Kwa upande wa Kadinali, “ugaidi huu wote ambao umechukua udhibiti wa maeneo mengi unatia wasiwasi. Ilionekana kuwa jeshi lilikuwa likifanya kazi ya kurudisha udhibiti wa Jimbo lakini kwa bahati mbaya hii sio hivyo na vipindi hivi vinaendelea ambavyo ni vya kusikitisha sana.” Alieleza Katibu wa Vatican.