Kard.Parolin: wakulima lazima wasikilizwe na hitaji la mazungumzo
Vatican News
Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican alizunguzia kuhusiana na maandamano yanayoendelea nchini Italia na Ulaya yote kupinga gharama kubwa za uzalishaji, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari pembezoni mwamkutano katika Jumba la Borromeo, ambalo ni makao ya Ubalozi wa Italia anayewakilisha Vatican, Alhamisi tarehe 8 Februari 2024 kwa ajili ya kuadhimisha miaka 40 ya Mkataba uliotiwa saini mwaka 1984 na aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo Bettino Craxi na Katibu wa Vatican, Kardinali Agostino Casaroli.
Kuhusu maandamano yanayoendelea, Kardinali alitoa wito wa kufunguliwa kwa nia ya uendelevu wa makampuni madogo na ya kati, huku akitumaini pia suluhisho la Mashariki ya Kati likiwemo kuachiliwa kwa mateka, kusitishwa kwa mapigano na kuanza kwa mazungumzo. Kardinali alisema “Lazima zisikilizwe, kuwe na mazungumzo, uwazi wa mazungumzo kwa nia ya uendelevu wa makampuni madogo na ya kati na mustakabali wa maeneo ya vijijini! Ahadi ni kwamba mtu huyo kila wakati anawekwa katikati ya kila kitu, kwa hivyo heshima yake inalindwa na anaweza kuelezea mapendekezo bora kabisa.”
Kuhusiana na Mkataba ambao sio jambo la zamani, lakini pia la makadirio ya siku zijazo, Kardinali alisema ni mambo gani ambayo yanaweza kuendelezwa leo kuanzia yale yaliyoainishwa miongo minne iliyopita. Hata hivyo katika tukio sawa na mkutano kuhusu Tamko la nia kati ya Italia na Vatican kwenye makao makuu mapya ya hospitali ya Bambin Gesù liliwasilishwa ambalo alisema “Maombi ya operesheni hii yataainishwa kwa upande wa Italia na Vatican."
Kardinali Parolin vile vilekatika swali la waandishi wa habari pia aliakisi mzozo wa Mashariki ya Kati, ambapo suluhisho na makubaliano ya kurejeshwa kwa mateka mikononi mwa Hamas yanaonekana kuwa mbali. “Kuna mazungumzo yanaendelea. Bila shaka, haionekani kama matumaini yanatimia, matumaini haya yanayoibuka kila kukicha. Lakini tunatumaini kwamba tunaweza kufikia makubaliano na suluhisho polepole kwa kuachiliwa kwa mateka na usitishaji wa mapigano. Na kisha kuanza kwa mazungumzo ya suluhisho la uhakika la tatizo.” Kardinali Parolin pia aliulizwa swali na waandishi wa habari kuhusu kesi ya kisheria inayomhusisha Gabriele Visco, mtoto wa waziri wa zamani Vincenzo Visco, ambapo jina la Parolin lilitajwa, yeye alisema: “Sawa anatoa maoni kwa maneno ya gazeti: haya ni majivuno ambayo hayapaswi kupewa uzito.”