Kardinali Parolin katika afla ya kumbu kumbu ya miaka 40 ya makubaliano ya Laterano. Kardinali Parolin katika afla ya kumbu kumbu ya miaka 40 ya makubaliano ya Laterano.  (ANSA)

Nchi Takatifu,Kard.Parolin:hasira kwa mauaji,ujasiri unahitajika kwa suluhisho

Katibu wa Vatican,pembezoni mwa afla katika Ubalozi wa Italia na Vatican kwa ajili ya kumbukumbu ya Makubaliano ya Lateran,alitoa maoni yake kuhusu hali ya Gaza: tunaomba kwamba haki ya Israel ya kujitetea ambayo iliombwa ili kuhalalisha operesheni hii iwe sawia na kwa hakika na usawa wa vifo elfu 30.

Na  Angella Rwezaula - Vatican.

Kardinali Pietro Parolin,  Katibu wa Vatican amenukuu maneno ya Mtakatifu Augustino  ili kutoa maoni yake juu ya hali ya Mashariki ya Kati, hasa huko Gaza, ambapo kwa  vifo elfu 30 kuna kile alichofafanua kama mauaji na pia kuomba suluhisho la haraka. Kardinali akiwa anaongoza  ujumbe wa Vatican alasiri Jumanne , tarehe 13 Februari 2024, kwa ajili ya mkutano wa kiutamaduni wa nchi mbili ili kuadhimisha kumbu kumbu ya Mkataba wa Lateran, ambao sasa unaadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake, mwishoni mwa mkutano ambao ulihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana  Sergio Mattarella na Waziri Mkuu Giorgia Meloni, alielezea hali ya Nchi Takatifu.

Kardinali Parolin katika afla ya kumbu kumbu ya miaka 40 ya makubaliano ya Laterano
Kardinali Parolin katika afla ya kumbu kumbu ya miaka 40 ya makubaliano ya Laterano

Kardinali lieleza  juu ya upande mmoja, dharau na  kwa upande mwingine, tumaini, akijibu maswali ya waandishi wa habari, pembeni mwa mkutano huo huko akiorodhesha mada zilizojadiliwa katika mazungumzo marefu nyuma ya milango iliyofungwa ikiwa ni pamoja na mwisho wa maisha, sera za familia na kuthamini posho moja, Imu, Jubilee na, bila shaka, migogoro inayoikumba dunia hii. “Pamoja na Rais wa Jamhuri na pia na Waziri wa Mambo ya Nje, muhtasari ulitolewa wa hali zote za shida ambazo kwa sasa zinasumbua ulimwengu na kuna hata wasiwasi kwa upande wa Italia na Vatican  alielezea Kardinali. “Ni vigumu zaidi kupata ufumbuzi wa matatizo haya, lakini tunajaribu kutoa mchango ambao unaweza kuwa chanya na kuanzisha njia za kuelekea amani.”

Kardinali Parolin na Rais wa Nchi ya Italia
Kardinali Parolin na Rais wa Nchi ya Italia

Waziri wa Mambo ya Nje mwenyewe, Antonio Tajani, tarehe 13 Februari  alizungumza kuhusu mwitikio usio na uwiano kwa upande wa Israel katika Ukanda huo. Italia, kwa hivyo, inaonekana kuungana na kile,  ambacho Kardinali Parolin alisema, “sauti ya jumla na kwamba hatuwezi kuendelea hivi. Tunahitaji kutafuta njia nyingine za kutatua tatizo la Gaza, tatizo la Palestina” - alisema Waziri wa Mambo ya Nje -. Vatican  imesema tangu mwanzo: kwa upande mmoja, hukumu ya wazi na isiyozuiliwa ya kile kilichotokea tarehe 7 Oktoba, na ninarudia hapa; hukumu ya wazi na isiyozuiliwa ya kila aina ya chuki dhidi ya Wayahudi, na ninairudia hapa. Lakini wakati huo huo pia ombi kwamba haki ya utetezi ya Israeli ambayo ilitolewa ili kuhalalisha operesheni hii ilingane na kwa hakika na vifo elfu 30 hailingani. Suluhisho la mzozo kwa sasa linaonekana kuwa mbali, lakini, Parolin alisema, "lazima tusikate tamaa. Mtakatifu Augustino alisema matumaini yanatokana na hasira na ujasiri, naamini sote tunakerwa na tukio hili la mauaji lakini tuwe na ujasiri wa kusonga mbele na tusikate tamaa kwani tukipoteza matumaini tunakumbana na mkono. Badala yake tunahitaji kupigana hadi mwisho na kujaribu kutoa mchango wetu, mchango wetu kadri tuwezavyo."

Kardinali Parolin akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje Bwana Antonio Tajan
Kardinali Parolin akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje Bwana Antonio Tajan

Akihimizwa na waandishi wa habari, kadinali huyo kisha akatoa taarifa kuhusu matokeo ya mkutano wa nchi hizo mbili na serikali: "Ilienda vizuri sana, kwetu sisi katika ujumbe wa Vatican na nadhani pia kwa wajumbe wa Italia ulikuwa mkutano mzuri sana, tuliweza kugusa baadhi ya masuala na mengine hata kuyachunguza kwa undani zaidi." Zaidi ya mada zote za "Kiitaliano", alisema: familia na masharti ya familia, kwa kutambua kile ambacho serikali imefanya kama posho moja kwa watoto, lakini bila shaka kuna nafasi ya kuingilia kati." Kisha mada ya shule za kibinafsi na pia mwisho wa maisha. Kuhusu suala hilo la mwisho, Kadinali huyo alieleza: "Tumegundua kwamba mikoa inajaribu kukabiliana na ukosefu huu wa sheria kwa upande wa Italia kwa matatizo ya aina hii lakini hakuna ufumbuzi". Suala la IMU pia liko mezani, katika suala hilo  pia Parolin alisema: "Hapa sio suala la kufikia hitimisho lolote. Tukio la Makubaliano ya Lateran ni zaidi ya kitu kingine chochote wakati ambapo hali hiyo inazingatiwa. Jambo zuri ni utayari wa kushirikiana na kufuatilia masuala haya."

Kardinali Parolin
14 February 2024, 17:46