Papa amteua Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Uchumi Dk.Benjamín
Vatican News
Alhamisi tarehe Mosi Februari 2024, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Katibu Mkuu Sekretarieti ya Uchumi Vatican, (SPE) Dk. Benjamín Estévez de Cominges, ambaye hadi uteuzi huo alilikuwa Mjumbe kwa ajili ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji katika Sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mahalia. Ameaona na ana Watoto watatu. Dk. Benjamín Estévez de Cominges alizaliwa tarehe 15 Aprili 1974. Alipata Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Usimamizi kutoka Shule ya Usimamizi ya Sloan ya Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (Marekani ya Amerika). Alihitimu katika Uhandisi wa Juu kutoka Chuo Kikuu Katoliki cha Leuven (Ubelgiji), na katika Uchumi na kisha katika Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Elimu cha Distancia (Hispania). Alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Comillas(Hispania). Tangu tarehe 17 Desemba 2021 amekuwa Mjumbe wa Utawala Baraza la Kipapa la Uinjilishaji katika Sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mahalia.
Akihojiwa kuhusiana na uteuzi hilo Estévez de Cominges alisema: “Imekuwa karibu miaka miwili ya pekee na yenye nguvu sana katika uongozi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu hapo awali, na sehemu ya pili ya Baraza la Kipapa Uinjilishaji baada ya kuchapishwa kwa Katiba Mpya. Ukweli wa kufanya uzoefu katika shirika hili kabla na kuwasili makao makuu ya Kipapa, bila shaka, ni wa msaada mkubwa, ingawa lazima nikiri kwamba utata wa Vatican ni mkubwa zaidi kuliko nilivyotarajia na, ingawa hii inafanya kuvutia zaidi, inahitaji muda wa kuzoea hali ambayo, kwa unyenyekevu, lazima niseme sijui ikiwa bado nimeshinda.”
Kwa maelezo ya Bwana Maximino Caballero, aliyekuwa Katibu Mkuu wa SPE aliyemaliza muda wake kuwa “Nimepata fursa ya kujua na kufanya kazi kwa karibu na Benjamín tangu kuteuliwa kwake kama Mjumbe wa Propaganda Fide, nilipokuwa na wadhifa sawa na Katibu Mkuu wa SPE. Katika kipindi hiki niliweza kutazama dhamira yake, taaluma yake na usahihi wake katika usimamizi, na vile vile tabia yake ya ushirikiano, ya upatanisho na ya maelewano na vyombo na na mabaraza mengine ya kipapa Ili kuhakikisha mpito unaofaa unaoruhusu kuendelea kwa baadhi ya mipango inayoendelea, Estévez de Cominges atapatanisha kwa muda msimamo wake wa sasa na ule wa Katibu Mkuu wa SpE.
Katibu mpya alisema: “Wakati Mkuu wa SpE alipopendekeza jukumu hili jipya kwangu miezi michache iliyopita - nilielewa umuhimu wake, lakini wakati huo huo nilionesha wasiwasi wangu juu ya kuacha Baraza iliyo wazi iliyozama katika mchakato wa mabadiliko makubwa ambayo yanaanza kuzaa matunda. Ninamshukuru sana Mkuu wa SpE kwa kunipa nafasi hii na Kardinali Tagle kwa ukarimu wake wa kuniruhusu kuondoka. Ninaamini kwamba kujua ukweli na utendaji wa Baraza la Kipapa inaweza kuwa muhimu sana kwa jukumu langu jipya, kusambaza mahitaji yake moja kwa moja ili kutoa huduma nzuri kutoka kwa Sekretarieti ya Uchumi. Ninajua kwamba jukumu ni kubwa na ninatumai kuwa nitatimiza kazi hii mpya kwa msaada wa Mungu na usaidizi wa familia yangu.”
Ikumbukue Sekretarieti ya Uchumi mjini Vatican, SPE, inaratibiwa na Baraza la Uchumi la Vatican lililoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 24 Februari 2014 kama sehemu ya mchakato wa mageuzi makubwa katika Sekretarieti kuu ya Vatican. Vigezo muhimu vinavyozingatiwa ni: huduma makini, ukweli, uwazi na nidhamu katika matumizi ya rasilimali fedha za Kanisa ambazo kimsingi ni kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia furaha ya Injili kwa watu wa Mataifa. Kumekuwepo na mafanikio makubwa katika mchakato wa kuandaa bejeti ya Vatican na taasisi zake. Udhibiti wa matumizi ya fedha za Kanisa utaendelea kufanyika ili kuhakikisha kwamba, kiwango cha bajeti kilichotengwa kinaheshimiwa kama sehemu ya maboresho ya huduma kwa watu wa Mungu kwa kuzingatia nidhamu, tija, weledi na ufanisi bora.