Makubaliano kati ya Italia na Vatican ya Hospitali ya Bambin Gesù huko Forlanini
Vatican News
Makao makuu ya kihistoria ya Mtakatifu Onofrio hayana nafasi tena ya upanuzi zaidi au kutoa maboresho katika utoaji wa huduma za afya au shughuli za utafiti. Na kwa hivyo Hospitali ya Kipapa ya Bambin Gesù inafanya ufunguzi wa kituo kipya katika eneo lililokuwa la Hospitali ya Carlo Forlanini katika siku zijazo. Hosptali hiyo ilizinduliwa katika miaka ya 1930 kama muundo wa kwanza mkubwa ulimwenguni uliojitolea kwa ajili ya matibabu ya kifua kikuu tu na kisha kubadilishwa kwa miongo kadhaa kuwa hospitali ya pande zote, hadi kufungwa kwake mnamo 2015.
Ubora kabisa
Kwa njia hiyo saini za Tamko la Nia moja ziliwekwa alasiri tarehe 8 Februari 2024 kati ya Kardinali Pietro Parolin, katibu wa Vatican na Katibu Msaidizi wa Urais wa Baraza Alfredo Mantovano (Italia) katika hafla ya kando ya Mkutano wa kuadhimisha miaka 40 ya (Concordat' yaani Mkataba) wa serikali ya Italia na Vatican ambapo imeamua kuipatia Hospitali ya Watoto eneo jipya la kufanyia shughuli zake, ambalo maelezo ya pamoja yanafafanua kuwa ni mafanikio kamili katika uwanja wa huduma ya afya ya watoto na utafiti wa matibabu, katika kiwango cha kitaifa na kimataifa.
Hatua za kuchukua
Ili kuanza mchakato utakaopelekea Hospitali ya Bambin Gesù kufanya kazi katika muundo wa zamani wa Forlanini, uliotambuliwa kama mojawapo ya sehemu zinazofaa zaidi kwa ujenzi wa makao makuu mapya, kwa muijibu wa taarifa tunasoma kuwa: “Azimio hilo linaweka malengo ambayo wahusika sasa watalazimika kufanya kazi, kuanzia ufafanuzi wa usanifu muhimu wa udhibiti ambao unapendelea utekelezaji wa hatua na uendelevu kamili wa kiuchumi wa operesheni.” Kwa maneno madhubuti, imeelezwa, hatua zitakazochukuliwa kuwa zitakuwa upatakanaji, bei itakayoanzishwa na Vatican ya eneo na mali inayoitwa ‘Forlanini complex’ kutoka Mkoa wa Lazio; kibali cha Vatican kwa kufikia haki ya juu zaidi, kwa muda na thamani itakayokubaliwa kati ya wahusika; ujenzi wa hospitali mpya na INAIL; ukodishaji wa INAIL wa jengo jipya la hospitali, kwa kuzingatia ada ambayo hulipa uwekezaji wa INAIL; hatimaye masharti ya makubaliano kati ya Vatican na Italia kwa uhamisho wa kinga zilizorejea katika vifungu. 15 na 16 ya Mkataba wa Lateran kwa makao mapya ya Hospitali ya Bambin Gesu’. Azimio hilo linarejea kuanza kwa majadiliano kati ya wahusika juu ya marudio ya jengo la kihistoria la Mtakatifu Onofrio, kwa kuzingatia kazi ya sasa ya ustawi wa jamii tata hiyo na pia kutoa haki ya kabla kwa niaba ya serikali ya Italia,”taarifa inahitimishwa.
Mantovano:lengo, kufungua makao makuu mapya ifikapo 2030
Akiongea na waandishi wa habari juu ya yaliyomo katika Azimio hilo, Katibu Mantovano alisema kuwa: “uamuzi wa pamoja ni matokeo ya shauku ya pamoja ya kutoa nafasi za kutosha kwanza kabisa kwa watoto ambao wana magonjwa makubwa, kwa familia zao, kwa madaktari wanaowahudumia na shughuli za utafiti.” Aliongeza kuwa “ ni njia tata kabisa kutoka kwa mtazamo wa kisheria na kiuchumi, lakini ambayo inaheshimu kikamilifu roho ya (Concordat)Mkataba, na kuishi pamoja kiukweli tofauti ambao hata hivyo hufuata nia sawa, kwanza ya utunzaji wote wa walio dhaifu zaidi.” Kusudi, alihitimisha Mantovano, “ni kufungua hospitali ifikapo 2030 ili kutoa Hospitali ya Bambin Gesù nafasi angalau mara nne kuliko ya sasa ambayo leo hii alisisitiza, hairuhusu hospitali kukuza uwezo ambao inajulikana duniani kote.”