Mfuko wa Centesimus Annus utatuza utafiti kuhusu mazingira magumu
Vatican News
Udhaifu wa kazi. Kuelekea Maadili zaidi ya Kibinadamu), ni kitabu kilichoandikwa na Carolina Montero Orphanopoulos, ambacho alishinda toleo la VI la tuzo ya kimataifa ya “Uchumi na Jamii”, katika sehemu ya machapisho, yaliyohamasishwa na Mfuko wa Kipapa wa Centesimus Annus-Pro Pontifice. Afla ya tuzo itafanyika jijini Roma, Jumanne tarehe 27 Februari 2024 saa 10.00 jioni, masaa ya Ulaya, katika chumba cha Yohane Paolo II, katika Taasisi ya Maria Bambina, na itaongozwa na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, ambaye atatoa hotuba pia ya kufunga hafla hiyo. Sifa ya kazi kwa mshindi itatangazwa na Kardinali Reinhard Marx, Askofu Mkuu wa Munich na Freising, nchini Ujerumani na Rais wa majaji ya Tuzo.
Zawadi
Tuzo hiyo hutolewa kila baada ya miaka miwili katika machapisho yanayojikita na nyanja ya kiuchumi na kijamii ambayo yanajitokeza kutoa mchango wa awali katika kujifunza na kutumia Mafundisho Jamii ya Kanisa na ambayo ni ya mshikamano wa kimafundisho unaotambulika, na pia kwa ujumla kueleweka kwa umma. Katika sehemu ya udhamini ya mafunzo toleo la III, kila mwaka na limehifadhiwa kwa watafiti vijana walio chini ya miaka 35, washindi ni: Sebastian Panreck, “Athari ya Ujumuishaji wa Soko juu ya Tabia ya Haki, Westfälische Wilhelmsuniversität (Münster) na Andrea Roncella, “Baada ya Ubepari wa Wanahisa: Kusudi-Ahadi ya uandaaji, wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu (Milano).
Kazi kuhusu mazingira magumu
Carolina Montero Orphanopoulos ni mtafiti katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Silva Henríquez cha Santiago (Chile). Baada ya kuhitimu katika Taalimungu ya Maadili na Hatua za Maisha ya Kikristo alipata Shahada ya Uzamili katika maadili ya utafiti wa matibabu na kibiolojia(Bioethics). Kazi yake inachunguza hali ya mazingira magumu kama uwazi wa kimsingi wa mwanadamu, hali ya kupenyeza, yenye kuathiriwa na kubadilishwa katika mwingiliano na mazingira ya mtu, mwenyewe, wengine na kile kinachopitia kwake. Kazi ya kiufundi na kinidhamu inayofanywa na mwandishi inazingatia aina inayofafanuliwa kama “mhimili wa kimsingi wa ukuzaji wa maadili ya Kikristo ya kibinadamu zaidi.”
Katika barua inayoambatana na kitabu imebainishwa kuwa: “kilele cha ufunguzi huu ni Umwilisho, ambapo, kwa kudhani kuwa hatari ya kibinadamu katika uwepo wa mtu mwenyewe, Yesu anakuwa mtu wa kupenyeka, kufikika na mwenye huruma, si tu katika matukio muhimu ya maisha na huduma yake, kama vile Mateso, bali katika shughuli zake za kila siku na anthropolojia ya uhusiano.” Kulingana na mwandishi, “udhaifu ni muhimu kama kitengo cha kimaadili, kitaalimungu na kianthropolojia, na ujumuishaji wake katika taalimungu ya kisasa ya maadili ni kazi ya kimsingi na ya dharura.”
Majadiliano katika meza ya mduara
Afla ya utoaji tuzo, ambayo itafunguliwa na Anna Maria Tarantola, rais wa Mfuko, pia inajumuisha meza ya mduara yenye kichwa “Athari za Mazingira Hatarishi kwa Nchi, Makampuni na Jamii.” Mwandishi wa habari Fabio Bolzetta, rais wa WECA (Chama cha Mitandao Kikatoliki cha Italia), atasisimamia. Hotuba zinatarajiwa kutoka kwa Sr Helen Alford, O.P., rais wa Chuo cha Kipapa cha Sayansi; Gregorio De Felice, mwanauchumi mkuu na Utafiti Mkuu, Banki ya Intesa Sanpaolo; Flavio Felice, profesa wa Historia ya Mafundisho ya Kisiasa katika Chuo Kikuu cha Molise; Elena Marta, profesa kamili wa Saikolojia ya Kijamii na Jamii, katika Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, Brescia Milano, Italia.