Bendera ya Umoja wa Mataifa Bendera ya Umoja wa Mataifa  (©Negro Elkha - stock.adobe.com)

Mons.Balestrero:Udharura wa mzozo wa kulipa deni nchi zinazoendelea

Vatican itaendelea kufanya kazi na UNCTAD na mashirika mengine ya kimataifa ili kukuza usanifu wa kifedha endelevu,usawa,uthabiti na unaolenga maendeleo.Mfumo kama huo unaweza kufikiwa tu wakati washiriki wote wa familia ya binadamu wamejumuishwa katika kutafuta manufaa ya wote na kuchangia katika hupatikanaji wa soko la kimataifa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu Ettore Balestrero, Mwakilishi wa  Kudumu wa Vatican  katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Taasisi Maalum huko Geneva na Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO), wakati wa kikao cha 75 cha Baraza la Biashara na Maendeleo ya Unctad huko Geneva, Uswiss, Jumanne tarehe  13 Februari 2024 alitoa tamko lake. Katika tamko alisema kuwa Ujumbe wake unakaribisha ripoti ya Biashara na Maendeleo: Ukuaji, Madeni, na Hali ya tabianchi, ambapo haja ya kushughulikia kushindwa kwa usanifu uliopo wa kifedha duniani kuwezesha ukuaji wa uchumi jumuishi na kutoa msaada wa kutosha kwa nchi zinazoendelea unasisitizwa. Askofu Mkuu alisema inatia wasiwasi mkubwa kwamba “ukuaji katika takriban kanda zote kwa mwaka wa 2023 na 2024 […] unatarajiwa kushuka chini ya wastani kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya janga hili la ulimwengu wa kisasa, na masoko ya fedha yasiyodhibitiwa na taasisi zenye upeo wa muda mfupi ni kichocheo cha mwelekeo huu mbaya.

Suala la kulipa deni 

Ripoti inaonesha udharura wa kushughulikia mzozo unaoibuka wa kulipa deni kwa nchi zinazoendelea, ambazo jumla ya deni la umma limeongezeka karibu mara mbili, na kufikia asilimia 64 ya Pato la Taifa wakati wa  2022, kanuni, inaweka mipaka ya uhuru wa kisera wa nchi zinazoendelea na uwezo wao wa kukusanya rasilimali ili kukidhi kupanda kwa gharama za changamoto zinazohusiana na hali ya tabianchi. Katika ukweli kwamba watu bilioni 3.3 wanaishi katika nchi ambazo pesa nyingi zinatumika kulipia deni la nje kuliko elimu au huduma ya afya ni hali isiyokubalika. Katika  Waraka wake wa  Fratelli Tutti, (Wote ni Ndugu) Papa Francisko anaonya kwamba mtindo wetu wa sasa wa kiuchumi “huimarisha utambulisho wa walio na nguvu zaidi, ambao wanaweza kujilinda, lakini unaelekea kupunguza utambulisho wa kanda dhaifu na maskini zaidi, na kuzifanya kuwa hatari zaidi na tegemezi. Kwa njia hiyo, maisha ya kisiasa yanazidi kuwa tete mbele ya nguvu za kiuchumi za mabadiliko zinazofanya kazi kwa kanuni ya ‘kugawanya na kushinda.’”

Mwingilia wa changamoti za kiuchumi na tabianchi

Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican aidha alisema kuwa , Ujumbe wake unatoa wito kwa UNCTAD, Nchi Wanachama, na wadau husika kuongeza juhudi za kushughulikia udhaifu wa kimuundo wa usanifu wa kimataifa wa kifedha, ambao unachangia kuongezeka kwa ukosefu wa usawa na kuziweka nchi zinazoendelea kwenye matokeo ya dhiki ya madeni na kifedha kutokuwa na utulivu. Kuongezeka kwa mwingiliano changamano kati ya hatari za kiuchumi, hali ya tabianchi na kijiografia kunahitaji mtazamo wa kimaadili kwa maendeleo, kwa nia ya kukuza utawala mpya wa kimataifa unaowezesha fedha na masoko “kuhudumia maslahi ya watu na manufaa ya pamoja ya binadamu.”

Vatican na UNCTAD

Vatican  itaendelea kufanya kazi na UNCTAD na mashirika mengine ya kimataifa ili kukuza usanifu wa kifedha endelevu, usawa, uthabiti na unaolenga maendeleo. Mfumo kama huo unaweza kufikiwa tu “wakati washiriki wote wa familia ya binadamu wamejumuishwa katika kutafuta manufaa ya wote na wanaweza kuchangia katika hilo la upatikanaji wa soko la kimataifa. Kwa kukazia zaidi alisema ni lazima tufanye kazi pamoja ili kujenga usanifu wa fedha wa kimataifa unaojumuisha na wenye ubunifu, unaolengwa kulingana na mahitaji maalum na vipaumbele vya LDCs, na wenye uwezo wa kusaidia maendeleo yao, kwa manufaa ya mwisho ya jumuiya nzima ya kimataifa. Hata hivyo, mshikamano unasalia kuwa msingi wa kujitolea upya katika kuwasaidia wale ambao wamepambana na changamoto za kifedha kwa miongo kadhaa, na mwongozo kwa wahusika wapya katika uwanja huu.

Vatican inaunga mkono mahitaji ya maendeleo ya kuondoa kaboni

Hatimaye, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican alisema  harakati za kukabiliana na hali ya tabianchi zinapaswa kuwa fursa ya kupatanisha vipaumbele vya mazingira na maendeleo na kutafakari hili katika kiwango cha fedha kinachopatikana kwa nchi zinazoendelea, kushughulikia mahitaji yao ya maendeleo na malengo yake ya  za uondoaji wa kaboni. Kwa maana hiyo, Vatican inaunga mkono juhudi za kuwezesha nchi zinazoendelea kutumia nafasi ya sera kwa ajili ya mabadiliko ya kimuundo na kukabiliana na hali ya tabianchi.

Hotuba ya Balestrero
14 February 2024, 16:58