Tafuta

Utekaji nyara kwa wakristo na mauaji ya huko Kafanchan nchini Nigeria (2022.12.23) Utekaji nyara kwa wakristo na mauaji ya huko Kafanchan nchini Nigeria (2022.12.23) 

Nigeria:Utekaji nyara,Nigeria haujadhibitiwa:mshikamano wa Baraza la Uinjilishaji

Katika nyakati hizi ngumu,Baraza la Kipapa la Uinjilishaji linatoa mshikamano wake wa ndani na wa dhati kwa watu wa Nigeria,wakikabiliana na shida ambayo inazidi kuongezeka na kwa kiasi kikubwa.Hayo yamo katika Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji kitengo cha Unilishaji wa Kwanza,Askofu Mkuu Nwachukwu kwa Askofu Mkuu Iwejuru wa Owerri na rais wa Baraza la Maaskofu la Nigeria.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katibu Mkuu wa Baraza la Uinjilishaji, Kitengo cha uinjilishaji wa kwanza, Askofu mkuu Fortunatus Nwachukwu, mwenye asili ya  Nigeria ilionesha mshikamano wake binafsi na Kanisa na wakazi wa Nigeria katika kujifunza kwa masikitiko kutoka vyanzo mbalimbali vya habari kuhusu mara kwa mara utekaji nyara nchini Nigeria, hali ambayo imekuwa mbaya zaidi katika siku za hivi karibuni. Askofu mkuu alisema “Katika nyakati hizi ngumu, Baraza la Kipapa linatoa mshikamano wake wa ndani na wa dhati kwa watu wa Nigeria, wakikabiliana na shida ambayo inazidi kuongezeka na kwa uwiano,” Miongoni mwa wale ambao wanajikuta katika mzozo wa vitendo hivi vya kulaumiwa ni mapadre, ,Watawa na waamini walei alisisitiza Askofu Mkuu Nwachukwu katika ujumbe uliotumwa kwa Ugorji, askofu mkuu Lucius Iwejuru wa Owerri na rais wa Baraza la Maaskofu la Nigeria. 

Unyanyasaji wa kimwili na uhalifu wa utekaji nyara

“Hakuna kinachoweza kuhalalisha uhalifu wa utekaji nyara” alisema Askofu  Nwachukwu kwa sababu “unyanyasaji wa kimwili na mateso ya kiakili yanayoambatana na utekaji nyara hudhoofisha nguzo za maelewano ya kiraia na kijamii, kwani yanatia kiwewe watu wanaohusika, familia zao na jamii kwa ujumla. “Mawazo na sala zetu zinaelekezwa kwa Maaskofu, mapadre na watawa, waseminari, washiriki waaminifu wa Kanisa, Wakristo wote na watu wenye mapenzi mema katika taifa zima,” unaendelea ujumbe ambao ndani yake unaoneshwa “hisia ya kina ya huruma kwa wahanga wasio na hatia wa utekaji nyara huu na familia zao. Sawa, na hiyo tunatoa wito kwa Serikali ya Nigeria kuchukua hatua haraka kushughulikia tishio hili na kukomesha mzozo unaoendelea.” Askofu Nwachukwu anatumaini kwamba “pamoja na kuchukua hatua za kulinda maisha na mali, Serikali, kwa kuungwa mkono na Kanisa, litafute njia za kuliweka upya taifa katika njia ya ukuaji wa uchumi, utulivu wa kisiasa na mafungamano ya kidini. Tumaini letu ni kwamba Kwaresima hii itaonesha matunda ya kiroho kwa kila mwamini na kila jumuiya ya kikanisa nchini Nigeria. Bwana awabariki na awalinde, Maria, Malkia na Msimamizi wa  Nigeria.Alihitimisha

Kwa miaka Nigeroa inakubwa na janga la utekaji nyara

Kwa miaka mingi, Nigeria imelazimika kukabiliana na janga la utekaji nyara ambao unalenga, pamoja na mapadre na watawa,  wageni, wafanyabiashara, wanasiasa, maafisa wa serikali, wanadiplomasia, watawala wa jadi, pamoja na raia wa kawaida wakiwemo wanafunzi na watoto wa shule, mara nyingi waathriwa wakati wa ibada za misa ndipo utekanji nyara unawakuta. Si rahisi kutofautisha kati ya utekaji nyara unaofanywa na vikundi vya kigaidi au vikundi vya wahalifu vinavyojaribu tu kupata faida ya kiuchumi. Iwe umefanywa na magaidi au majambazi, baadhi ya aina tofauti za utekaji nyara zimeorodheshwa: utekaji nyara uliopangwa wa watu mahususi, waliotambuliwa hapo awali; utekaji nyara wa nasibu, haswa barabarani, kuchukua wahasiriwa bila mpangilio; utekaji nyara mkubwa (pamoja na uvamizi unaopangwa kwa ujumla kwenye vijiji, mahali pa ibada, ikijumuisha makanisa na misikiti, shule, treni na vituo vya reli).

Utekaji nyara umekithiri

Katika “kesi ya utekaji nyara wa waathiriwa waliochaguliwa kwa usahihi, tumegundua utekaji nyara wote kwenye njia ya kawaida ya mtu anayetekwa nyara, na vile vile mashambulizi ya usiku nyumbani, na mitego ya hisia (Mtego wa Asali), ili kumvuta mwathirika mahali ambapo atatekwa nyara.” Nchini Nigeria tangu Mei 2023 na mwanzo wa mamlaka ya Rais Bola Ahmed Tinubu, kampuni ya ushauri ya usimamizi wa hatari ya (SBM) imerekodi kutekwa nyara kwa watu 3,964. Utekaji nyara huo haujaacha mji mkuu wa shirikisho la Abuja, ambapo mnamo Januari 5 Mansoor Al-Kadriyar alitekwa nyara pamoja na mabinti zake sita. Mwanamume huyo aliachiliwa baadaye ili kulipa fidia ya naira milioni 50 zenye thamani ya dola (35,336) kwa ajili ya kuwaachilia binti zake. Mmoja wa hawa aliuawa kufuatia kushindwa kulipa kiasi kilichoombwa. Hata hivyo, wale wengine walipata tena uhuru wao baada ya kulipa fidia. Mnamo Januari 11,2024 katika eneo la mji mkuu wa shirikisho, watu wenye silaha waliovaa sare za kijeshi walifanya utekaji nyara mkubwa, na kuwateka nyara watu 11. Mmoja wao, msichana mwenye umri wa miaka 13, aliuawa kwa kushindwa kulipa fidia. Mnamo Januari 18,2024  jumba la kijeshi la Kurudu lilishambuliwa hata na utekaji nyara wa watu wawili.

Mshikamano wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji kwa Nigeria
16 February 2024, 16:30