Tafuta

Makubaliano kati ya Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto na Chuo Kikuu cha Santa Croce(Msalaba Mtakatifu). Makubaliano kati ya Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto na Chuo Kikuu cha Santa Croce(Msalaba Mtakatifu). 

Nyanyaso:makubaliano kati ya Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto na Santa Croce

Makubaliano ya ushirikiano yalitiwa saini mnamo Februari 7 na Kadinali O'Malley na Mkuu wa chuo kikuu,Padre Luis Navarro.Chuo kikuu cha Santa Croce kitaweza kuandaa kozi za mafunzo kwa walimu,wanafunzi na wafanyakazi wa taasisi ya Vatican.Gambera:ni furaha kuwa katika huduma ya juhudi muhimu katika Kanisa.

Vatican News

Kardinali Sean O'Malley alitia saini ya Mkataba kati ya Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Santa Croce (Msalaba Mtakatifu), Jumatano tarehe 7 Februari 2024 ambapo alisema kuwa: “Makubaliano haya  ni sehemu ya makubaliano ya ushirikiano ambayo Tume inatia saini na mashirika mengine ya kikanisa ili kutekeleza utume wake.”

Vifungu vya Mkataba

Hati hiyo,iliyosainiwa huko nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican na rais wa Tume na Mkuu wa Chuo kikuu cha Santa Croce,(Msalaba Mtakatifu) Padre Luis Navarro, inatoa,  ushirikiano katika dhamira ya pamoja ya kuzuia unyanyasaji na ulinzi wa watoto na watu wazima walio katika mazingira magumu kawaida. wa Kanisa la Ulimwengu”. Hasa, Chuo Kikuu cha Santa Croce (Msalaba Mtakatifu) kitaweza kuwa mwenyeji wa mipango inayohusishwa na utume wa Tume ya Vatican na kuhimiza maandalizi ya semina, kozi za mafunzo kwa walimu, wanafunzi na wafanyakazi wasio waalimu, pamoja na shughuli za mafunzo zinazoendelea kwa wafanyakazi wa Tume au mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari katika Tume hiyo hiyo ya Kipapa.

Kuandaa ripoti za kila mwaka

Taasisi hizo mbili, kwa mujibu wa taaraifa inabainisha kuwa, “zinapanga kuandaa ripoti ya kila mwaka juu ya mipango iliyofanywa, ambayo inaweza kutangazwa kwa umma kupitia njia zao. Ushirikiano huo ni halali kwa miaka mitatu na unaweza kufanywa upya.” Gambera alijibu shukrani za Kardinali O'Malley kwa chuo kikuu kwamba: “Tuna furaha kuwa katika huduma ya juhudi muhimu na ya pamoja ndani ya Kanisa.”

Makubaliano ya Kozi kuhusu ulinzi wa Watoto na Chuo Kikuu cha Santa Croce.
15 February 2024, 16:15