Panama,Kadinali Lacunza amepatikana: alitoweka mnamo Januari 30
Vatican News
Kardinali José Luis Lacunza Maestrojuán, wa Jimbo Daudi nchini Panama, mwenye umri wa miaka 79, alipatikana akiwa salama na mzima alasiri ya Alhamisi tarehe 1 Februari 2024, baada ya kutoweka tangu saa 8.00 mchana wa Jumanne tarehe 30 Januari 2024 tangu hapo alikuwa hajaonekana na hawakuwa na habari zozote. Habari hii imethibitishwa na barua fupi kutoka kwa Baraza la Maaskofu wa Panama (CEP) iliyochapishwa karibu saa 4.30 usiku(masaa ya Kiitaliano)ambayoinaripoti habari kutoka kwa mamlaka na kutoa shukrani kwa sala na maonesho ya mshikamano.
Na chapisho limeoneshwa Video iliyoshirikishwa kwenye jukwaa la kijamii linaonesha afisa wa polisi akizungumza kupitia dirisha la gari na Kardinali Lacunza, ambaye anampatia maji. Kardinali huyo alionekana “amechanganyikiwa, Askofu mkuu wa mji mkuu wa Panama, José Domingo Ulloa Mendieta, aliwaambia waandishi wa habari na kuarifu kwamba Kardinali Lacunza alikuwa amehamishwa kupokea matibabu katika hospitali ya Jimbo la Daudi
Hakuna habari kwa siku mbili
Habari za kutoweka kwa Kardinali Lacunza ambaye aliondoka nyumbani kwake majira ya alasiri bila simu, pochi wala sanduku, zilisambaa kwa taarifa rasmi ya Jimbo la Daudi ambalo, bila kutunga au kupendekeza dhana yoyote juu ya kutoweka, watu wa Mungu ambao Kadinali alikosekana rasmi tangu Jumanne Januari 30, 2024” Likiomba maombi kutoka kwa waumini ili mapema hara , mchungaji wa jimbo ao aweze kupatikana , pia lilipoti kuwa “limewasilisha malalamiko hayo kwa mamlaka ya Mwendesha Mashtaka wa Umma, ambaye alianza uchunguzi wa kesi hiyo mara moja.” Mwendesha mashtaka Javier Caraballo alikuwa amewathibitishia waandishi wa habari kwamba wachunguzi walikuwa wametumwa katika jimbo la Chiriquí, kwenye mpaka wa magharibi wa nchi ya Amerika ya Kati, ambako Jimbo la Daudi lipo. Caraballo pia aliongeza kwamba tulikabiliwa na ‘kesi tete’. Wizara ya Mambo ya Ndani pia ilihusika katika uchunguzi huo, ikisaidia polisi wa kitaifa na wa ndani.
Sala ya maaskofu na Kanisa la Panama
Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Panama (CEP), ambalo Lacunza alikuwa rais kwa vipindi viwili, baada ya kujua rasmi juu ya kupotea kwa ndugu yao, waliwahimiza watu wote wa Mungu kuungana katika sala ya kudumu, wakiomba kwamba kujua ni wapi anapatikana. Maombi pia yalishirikiwa na Jimbo kuu la Panama (ambalo Jimbo la Daudi liko ndani mwake) ambayo katika chapisho kwenye akaunti rasmi ya
Askofu Mkuu Ulloa: ushirikiano kati ya Kanisa na mamlaka
Askofu Mkuu Ulloa, akizungumza na waandishi wa habari asubuhi, alieleza kwamba mamlaka ya kikanisa yanachunguza pamoja na mamlaka ya kiraia ya Daudi: “Tutakuwa wazi iwezekanavyo ili tuweze kuwa na taarifa za kwanza juu ya kile kinachotokea.” Hadi wakati huo hakukuwa na taarifa za kina juu ya Kardinali: “Alitoka na mambo ya kawaida ya kufanya, baadhi ya kazi, na kisha kutoka huko hakuna kitu kingine kilichosikika hadi siku iliyofuata wakati kutokuwepo kwake kuligunduliwa. Kawaida huadhimisha Ekaristi,” alieleza Askofu Mkuu Ulloa, pia akiripoti kwamba upekuzi ulianza mara moja na washirika ambao walikuwa wamewatahadharisha makuhani wa Daudi.
Kardinali wa kwanza wa Panama
José Luis Lacunza Maestrojuán, mzaliwa wa Pamplona, Hispania, Mwanashirika wa Shirika la Waagostiniani, mwenye umri wa miaka 79, ni mchungaji wa Jimbo la David, mji mkuu wa jimbo la Chiriquí, eneo la tatu la mijini nchini Panama, ambapo karibu nusu milioni ya wakaazi na moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na karibu watu elfu 70 wa kiasili ambao Kardinali ameonesha uungwaji mkono, ulinzi na ukaribu kwao. Kuanzia 2000 hadi 2004 na kisha kutoka 2007 hadi 2013 alikuwa rais wa Baraza la Maaskofu la ndani. Pia alishika wadhifa wa kuwa katibu mkuu wa Sekretarieti ya Maaskofu wa Amerika ya Kati (Sedac) na mkuu wa sehemu ya kichungaji kwa utamaduni wa Baraza la Maaskofu la Amerika ya Kusini (Celam), ambalo tangu 2015 pia amekuwa rais wa Kamati ya Uchumi.
Mwaka 2015 Papa Francisko alimuumba kuwa Kardinali, na kupata kofia ya kwanza nyekundu kwa Kanisa la Panama na pia wa kwanza katika historia ya karne nyingi ya Shirika la Waagostiani. Mnamo 2019 Kardinali Lacunza alimkaribisha Papa nchini Panama katika Siku ya Vijana Duniani.
Sasisha la mwisho saa 4.45 usiku tarehe 1 Februari 2024