Papa amekutana na Bw,Mleli, Rais wa Jamhuri ya Argentina
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko asubuhi tarehe 12 Februari 2024, amekutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican, na Rais wa Jamhuri ya Argentina, Bwana Javier Gerardo Milei, ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Vatican, wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Wakati wa mazungumzo yao ya ukarimu katika Sekretarieti ya Vatican wameonesha kuridhika na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Vatican na Jamhuri ya Argentina na hamu ya kuyaimarisha zaidi. Na baada wakazingazia mpango mpya wa Serikali wa kukabiliana na msukosuko wa kiuchumi.
Wakati wakiendelea na mazungumzo yao, baadhi ya masuala ya kimataifa yaliguswa, hususan migogoro inayoendelea na kujitolea kwa amani kati ya mataifa. Katika mazungumo hayo vile vile wamegusia mada zenye tabia ya Kimataifa kwa namna ya pekee migogoro inayoendelea na jitihasa kwa ajili ya amani kati ya mataifa.
Zawadi kutoka kwa Baba Mtakatifu: Medali ya shaba iliyochochewa na kifuniko cha Altare ya Mtakatifu Petro. Idadi ya hati za upapa na Ujumbe wa Amani wa mwaka huu 2024.
Zawadi kutoka kwa Rais: Ishara ya posta iliyowekwa na Ofisi ya Posta ya Argentina kwa ajili ya Mama Antula ambaye ametangaza kuwa mtakatifu tarehe 11 Februari 2024. Nakala ya hati ambayo Serikali ya Argentina iliidhinisha ya Juan Bautista Alberdi kama Mkataba wa makubaliano ya Papa (1854) na hatimaye baadhi ya keki za kawaida za Argentina.