2024.02.15 Papa na Bwana  Ion-Marcel Ciolacu, Waziri Mkuu wa Romania 2024.02.15 Papa na Bwana Ion-Marcel Ciolacu, Waziri Mkuu wa Romania  (Vatican Media)

Papa Francisko akutana na Waziri Mkuu wa Romania

Baba Mtakatifu akikutana na Bwana Ion-Marcel Ciolacu,Waziri Mkuu wa Romania mjini Vatican,wamezungumzia juu ya uimarishaji wa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na kupitia upya masuala ya sasa katika uwanja wa kimataifa hasa Vita na wakimbizi.

Na Angella Rwezaula‘- Vatican

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Vyombo vya habari Vatican, imebanisha kuwa Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 15 Februari 2024  amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Romania, Bwana Ion-Marcel Ciolacu ambaye mara baada ya mkutano huo pia amekutana na Kardinali Pietro Parolin,  Katibu wa Vatican akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa.

Papa Francisko na ujumbe wa Waziri Mkuu wa Romania
Papa Francisko na ujumbe wa Waziri Mkuu wa Romania

Wakati wa mazungumzo yao na Sekretarieti ya Vatican wamesisitiza juu ya kuongezeka kwa hali  ya juu ya mahusiano mazuri kati ya Vatican na Romania na juu ya mitindo ya  ushirikiano wa juu katika sehemu zote mbili kwa ajili ya manufaa ya watu wa Romania hasa katika muktadaha wa Elimu. Baadaye, baadhi ya mada za maslahi ya pande zote na masuala ya sasa yaligusiwa ikiwa ni pamoja na mgogoro wa Israeli na Palestina na Ukraine, kupokea wahamiaji na wakimbizi, pamoja na matarajio ya upanuzi wa mpango wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Romani alikutana na Katibu wa Vatican
Waziri Mkuu wa Romani alikutana na Katibu wa Vatican

Katika kubadilishana zawadi, Baba Mtakatifu Francisko amempatia waziri Picha ya shaba inayoleza ‘Ukaribu’; Idadi ya hati za upapa; Ujumbe wa Amani wa mwaka 2024 na Kitabu kuhusu Statio Orbis cha tarehe 27 Machi, 2020 kilichohaririwa na LEV. Kitabu cha  Nyumba ya Kipapa ya Mikutano, iliyohaririwa na Mkuu wa  Nyumba ya  Kipapa. Wakati huo huo, Wziri Mkuu amemzawadia Papa Mchoro unaoonesha maaskofu saba wafiadini waliotangazwa kuwa wenyeheri na Papa Francisko mnamo mwaka wa 2019.

Papa akutana na Waziri Mkuu wa Romania
15 February 2024, 15:46