Papa amepokea barua na Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Peru
Vatican News.
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 16 Februari 2024 amepokea barua na hati za utambulisho wa Balozi kutoka Peru, Bwana Luis Juan Chuquihuara Chil. Alizaliwa tarehe 10 Novemba 1953 na ameoa ana watoto wanne.
Mafunzo yake ya Fasihi (1971 – 1972) na Sheria (1973 – 1976) katika Taasisi ya Kipapa. Shada ya Uhusiano wa Kimataifa katika Taasisi ya Kidiplomasia ya Peru (1979); Diploma ya Mafunzo ya Kisiasa katika Taasisi ya Mafunzo ya Kisiasa huko Paris, Nchini Ufaransa (1985 – 1986); Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Umma katika Taasisi ya Kimataifa ya Utawala wa Umma (IIAP), Paris, Ufaransa (1988-1989).
Aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Urais wa Jamhuri, Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Baraza la Urais wa Mahakama, na mshauri wa kisiasa wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri. Pia ameshika nyadhifa mbalimbali kama vile za ofisi za Urais wa Jamhuri, katika Mahakama, Wizara ya Mambo ya Nje, Chuo cha Diplomasia, Tume ya Taifa ya Maendeleo na udhibiti wa Dawa za Kulevya. Hadi uteuzi huo alikuwa Balozi na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa yenye makao yake makuu Geneva, Shirikisho la Uswisi, UNEP na UN-HABITAT, yenye makao yake makuu Nairobi, Kenya (2021-2024).