Papa Francisko amekutana na Waziri Mkuu wa Suo Tomé na Príncipe
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Alhamis tarehe Mosi Januari 2024 amempokea katika Mkutano kwenye Jumba la Kitume Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Suo Tomé na Príncipe, Bwana Patrice Émery Trovoada, ambaye baadaye amkutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akisindikizana na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu msaidizi wa Mahusiano na Nchi na Mashirikisha ya kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombyo vya habari Vatican, imebainisha kuwa wakati wa mazungumzo yao, walionesha mahusiano mazuri kati ya Vatican na Jamhuri ya Kidemokrasia ya São Tomé na Príncipe na kusisitiza juu ya mantiki ya hali za kisiasam kijamii na kiuchumi wa nchi hasa juu ya kushikiana katika uwanja wa elimu na afya. Wakiendelea katika mazungumzo yao kulikuwa hata na mabadilishano yam aoni juu ya hali ya sasa ya kimataifa kwa namna ya pekee juu ya matatizo ya usalama katika Nchi ya Bara la Afrika.
Katika Mkutano wa Papa ulionza saa 1:50 asubuhi na kuhitimishwa mazungumzo saa 2.10 asubuhi, ambapo baadaye walibadilishana zawadi kama kawaida ambapo Baba Mtakatifu Francisko amempatia mgeni wake sanamu ya shaba yenye kichwa: Mazungumzo kati ya kizazi. Vitabu vyenye hati za kipapa, Ujumbe wa amani kwa mwaka 2023 na hatimaye kitabu kuhusu Statio Orbis cha Njia ya msalaba ya tarehe 27 Januari 2020 kilichotayarishwa na nyumba ya vitabu ya Vatican LEV.