Papa amemteua Padre Jean Désiré Razafinirina kuwa Askofu wa Morombe,Madagascar
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Jumatatu tarehe 12 Februari 2024, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu wa Jimbo la Morombe nchini (Madagascar) Mheshimiwa sana Padre Jean Désiré Razafinirina, wa Jimbo la Toliara, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Gambera na Profesa wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji ya Vohitsoa.
Wasifu wake
Askofu Mteule Jean Désiré alizaliwa tarehe 5 Mei 1975 huko Manombo, Jimbo kuu la Toliara. Alijiunga na Seminari Kuu ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji huko Vohitsoa na baadaye akapata leseni ya sheria za kanuni za Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, Roma.
Alipewa daraja la Upadre tarehe 10 Agosti 2003 kwa ajili ya Jimbo kuu la Toliara.
Nyadhifa nyingine
Alishikilia nyadhifa zifuatazo: Profesa katika Seminari Ndogo ya Toliara, Padre huko Andranovory (2003-2004) na Paroko Kanisa Kuu (2004-2005); paroko wa Mama Yetu Mpalizwa huko Sakaraha (2005-2007); Paroko wa Kanisa Kuu la Toliara na Mjumbe wa Chuo cha Washauri (2010-2013); Mkufunzi katika Seminari Kuu ya Vohitsoa, Fianarantsoa (2013-2017); tangu 2017 amekuwa Gambera na Mlezi wa Seminari Kuu ya Vohitsoa,Fianarantsoa.