Safari kuelekea Jubilei na vipindi vya kila Juma vya RAI 1
Vatican News
Huduma, mahojiano na ripoti zitarejea historia yake lakini pia zitapendekeza safari katika ulimwengu wa kisasa, miongoni mwa vijana na sehemu mbalimbali, nchini Italia na nje ya nchi, ili kusimulia historia na kutoa sauti kwa mahujaji. Imetayarishwa na Televeshini ya Italia (Rai) ya Vatican, ambapo matangazo ya Kipindi hicho yaliwasilishwa Alhamisi tarehe 22 Februari 2024 katika mkutano na waandishi wa habari.
Kipindi cha kwanza kilitayarishwa “Mbele ya Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro,” ambacho kitatambulisha historia yake na kitahusu Jubilei za karne zilizopita. Ripoti itafuatilia wasifu wa hija, wakati kwa mtazamo wa kimataifa kwa kujaribu kuelewa wapi mahali pa kupata tumaini leo hii. Mgeni mkuu atakuwa Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti wa Baraza la Uinjilishaji.
Jubilei 2025 Mahujaji wa Matumaini
“jarida la kila Juma linalotayarishwa na Rai -Vatican na kusimamiwa na mkurugenzi wake Stefano Ziantoni, litatangazwa kuanzia Dominika tarehe 25 Februari 2024 wakati wa kipindi cha Rai1, saa 6.45 za usiku, na litapatikana kwenye Rai Play. Litatoa ushuhuda, mahojiano, huduma za kiutamaduni, ili kuwaambia wadadisi na kuanzia Septemba ijayo litakuwa tukio la kila siku. Matangazo hayo, yaliyowasilishwa tarehe 22 Februari 2024 jijini Roma katika mkutano na waandishi wa habari, yataturuhusu kukaribia Jubilei pia kupitia simulizi kutoka ulimwenguni, yatatoa sauti kwa mahujaji, yatachunguza katika mwaka huu wa maandalizi yaliyowekwa kwa ajili ya sala, kwa Utashi wa Papa Francisko, jinsi ya kusali katika mahali patakatifu, katika magereza, katika nyumba za watawa na watajaribu kuelewa jinsi gani vijana wanasali na kuna uhusiano gani kati ya sala na Akili Mnemba.
Jubilei pia ni utamaduni
Askofu Mkuu Fisichella alifafanua kuwa: “Uzalishaji wa awali na wa ubunifu, haifuatilii mifumo iliyojulikana tayari, lakini inatoa mwelekeo wa matarajio. Mpango ambao una ufunguzi wa kiutamaduni muhimu, kwa kuwa “Yubile ni utamaduni.” Mwenyekiti wa Uinjilishaji pia alisisitiza kwamba “taarifa za jumla ni za msaada mkubwa hasa kwa vikundi vya watu wachache ambavyo havina uwezekano mwingi wa kuhisi umoja katika imani”, akiongeza kusema jinsi ambavyo ukumu la vyombo vya habari ni muhimu leo hii. Akizungumza kwa vyombo vya habari vya Vatican , Askofu Mkuu Fisichella aliakisi jinsi ambavyo “kusubiri kuvuka Mlango Mtakatifu kunahitaji maandalizi ya kutosha, kwa sababu hiyo Papa Francisko alitaka kutanguliza Jubilei kwa mwaka wa sala, ili Mlango huo uweze kuakisiwa kwa maana ya ndani zaidi.”
Na kuhusu mchango ambao vyombo vya habari vinaweza kutoa, alieleza kuwa “ni chombo chenye maamuzi na kwa hiyo hawana uwezo wa kutoa habari tu, bali pia kuwasiliana na mahujaji, ambao kwa njia ya mawasiliano wanakuwa wahusika wakuu kwa sababu sio tu kwamba wanaweza kusimulia hisotria zao kwa wengine, lakini pia wanaweza kuwafanya waelewe thamani kubwa ya hija zao.
Programu ya ulimwengu
Jubilei 2025 ya Mhujaji wa Matumaini itakuwa kwa hiyo kipindi cha “kidunia” kwa mujibu wa mkurugenzi wa Rai - Vaticano, Stefano Ziantoni na kwamba inazungumza na kila mtu, na ambayo itahusisha sana vijana, washawishi.” Kipindi cha kwanza kitarejea wakati, hadi kwenye habari fulani za kwanza za Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Vatican iliyoanzia mnamo mwaka 1500, kwa Papa wa wakati ule Alexander VI, lakini pia itakumbusha baadhi ya maandiko ya kihistoria ambayo yanataja mlango uliofunguliwa katika Jubilei ya 1350 pamoja na Papa Clement VI na katika 'Mwaka Mtakatifu wa 1423, na pengine ule wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano.
“Kisha tutapiga hatua katika ulimwengu wa leo hii, tukiwa na maoni na matarajio ya watu kuhusu mwaka wa Jubilei. Mkuu wa Rai -Vatican alifafanua kwamba bidhaa ya televisheni ya haraka na yenye nguvu iliundwa, kijana, isiyochosha, inayotoa historia mpya na pia udadisi. Kwa hivyo, kwa mfano, “katika sehemu ya pili tutasikiliza historia ya mchongaji pekee aliye hai aliyeunda Mlango Mtakatifu, ule wa Mtakatifu Maria Mkuu,” na katika sehemu ya tatu tutakwenda, pamoja na Klabu ya Alpine ya Italia(CAI) ili kugundua misalaba 14 ya Jubilei iliyotangazwa na Papa Leo XIII katika vilele vingi." Alisisitiza mhusika huyo
Hata hivyo akiendelea na maelezo alisema kuwa "Kamera za Rai pia ziliingia kwenye kiwanda ambacho Mlango Mtakatifu, wa Mtakatifu Petro ulitengenezwa na kwa, Mfuko wa Mazingira wa Italia (FAI), zitaonesha maeneo yanayojulikana na yasiyojulikana sana, kama vile “ambapo koti la silaha ambalo waliweka juu ya mkate kwa ajili ya ushirika wa watu wa Byzantine”. Haya yote, yanaruhusu kuchanganya utamaduni, mazingira, historia na mengi zaidi,” alihitimisha Ziantoni.