WUCWO yandaa Mkutano wa Kiekuemene na kidini mtandaoni kwa Siku ya Wanawake
Vatican News
Shirikisho la Umoja wa Wanawake Wakatoliki ulimwengun (UMOFC-WUCWO) kwa kushirikiana na Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidin(DDI), katika kuelekea Siky ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 ya kima mwa, memandaa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa 2024 kwa njia ya kukutana kupitia njia ya Mtandao, siku ya Jumanne tarehe 5 Machi 2024 kuanzia alasiri saa 9.00 kamili hadi saa 10.30 jioni ma saa za Roma. Tukio hilo litawaleta pamoja wanawake wa imani kutoka mila na tamaduni mbalimbali za kidini ili kutafakari juu ya jukumu muhimu ambalo wanawake wa imani wanafanya katika kujenga utamaduni wa amani na kukutana. Wakiongozwa na ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Siku ya 56 ya Amani Duniani, hasa kwa maneno ya “hazina yetu kuu, ijapokuwa iliyo dhaifu zaidi, ni udugu wa kibinadamu, unaosimikwa katika umwana wa pamoja wa Kimungu, na kwamba hakuna awezaye kujiokoa peke yake” , tukio hilo litaakisi kwa hakika ubinadamu wa pamoja wa wote na uwajibikaji wa pamoja katika kukuza amani.
Wanawake ndio wanaoharibiwa zaidi katika hali ya vita
Katika hali ya vita na migogoro ambayo ulimwengu unapitia, wanawake na wasichana ndio walioharibiwa zaidi, wale wanaoteseka zaidi. Migogoro inayotokana na sababu za kisiasa au majanga ya hali ya tabianchi, mara nyingi huwaacha wanawake kwenye usukani wa familia zao, na kuwa ndio wanaobaguliwa zaidi. Kwa ujasiri na uwezo wa kusikiliza, wanawake wanaweza kuwa wajenzi wa amani na mazungumzo. Tukio hilo litaanza na hotuba ya ufunguzi ya Kadinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, MCCJ, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini(DID), na Mónica Santamarina, Rais wa Shirikisho la Umoja wa Wanawake Waakatoliki ulimwenguni(UMOFC-WUCWO)
Wazungumzaji wa dini mbalimbali kutoka pande zote za dunia
Ratiba ya pande zote itahuishwa na wazungumzaji kutoka asili tofauti za kidini: Rudina Collaku, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Wanawake cha Maendeleo na Utamaduni, kutoka Albania, kwa mada: “Kuzuia misimamo mikali miongoni mwa vijana.” Kwa mtazamo wa Wabuddha, Elena Seishin Viviani, makamu wa rais wa Muungano wa Wabuddha wa Italia, atazungumza juu ya: “Kuanzia amani ya ndani hadi katika jamii zenye amani: Jukumu la kutafakari.” Kwa mtazamo wa Kihindu, kutakuwa na hotuba ya Svamini Hamsananda Ghiri, makamu wa rais wa Umoja wa Wahindu wa Italia, kuhusu mada: “Mazungumzo ya kiutamaduni - Mtazamo wa tamaduni za mwenyeji.”
Atakaye wakilisha mtazamo wa Kiyahudi atakuwa Mkuu wa Kiyahudi Allyson Zacharoff wa Usharika wa Beth Hatikvah katika Mkutano wa NJ, Marekani, ambaye atazungumzia: “Mazungumzo ya kidini na upatanisho kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu.” Kwa mtazamo wa kiekumene, Dk, Kuzipa Nalwamba kutoka Baraza la Makanisa Ulimwenguni atakuwa mgeni, kwenye mada: “Jinsi wanawake, wanachama au viongozi wa jumuiya za Kikristo, walivyoshirikiana katika michakato ya amani”. Kwa mtazamo wa Kikatoliki, Dk. Valeria Martano kutoka Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na mshauri wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini atajikita na mada ya: “Amani inaonekanaje wakati wa vita?
Tukio hili litakuwa na maoni kutoka kwa wafadhili wa hafla hiyo: Florence Mangin, Balozi wa Ufaransa katika Mji wa Vatican; Chiara Porro, Balozi wa Australia katika Mji wa Vatican; Annemieke Ruigrok, Balozi wa Uholanzi katika mji wa Vatican. UMOFC imekuwa ikisherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa njia ya kidini tangu 2019, kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini tangu 2020. Mada zinazochaguliwa kila mwaka zinaonesha uadilifu wa Kanisa, na kupendelea mtazamo wa kidini.