Tafuta

Siku ya Watoto Duniani,kukumbatia watoto wadogo kutoka pembezoni mwa dunia

Toleo la kwanza la Siku ya Watoto Duniani liliwasilishwa katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican na litafanyika Roma tarehe 25 na 26 Mei 2024.Itaadhimishwa pia katika ngazi mahalia.Kardinali de Mendonça:Matakwa ya Papa ni mkutano huo uwe tukio la kawaida kwa Kanisa.Mratibu Padre Fortunato:tutapendekeza njia tatu za maandalizi,kiroho,mshikamano na kiutamaduni.

Vatican News

Je, siku moja kutakuwa na Siku ya Watoto Duniani? Lililikuwa ni la Mtoto Alesandro kwa  Papa  mwenye umri wa miaka 9,  ambaye alipata nafasi kati ya vijana katika mazungumzo na Papa Francisko katika Podcast iitwayo  Popecast, katika mkesha wa Siku ya vijana duniani (WYD). “Ingekuwa nzuri, ninaipenda sana,” Papa alikuwa ametoa  maoni,  huku akibainisha kuwa ni wazo zuri. “Nitafikiria juu yake na kuona jinsi ya kuifanya,” aliongeza.

Uwasilishaji wa Siku ya Watoto Duniani 25 na 26 Mei 2024
Uwasilishaji wa Siku ya Watoto Duniani 25 na 26 Mei 2024

Na majibu yake hayakuchelewa kufika. Papa Francisko  alikutana na zaidi ya watoto 7,000 kutoka duniani kote  mnamo tarehe 6 Novemba 2023  katika mpango wa “Tujifunze kutoka kwa wavulana na wasichana” na mwezi mmoja baadaye,  tarehe 8 Desemba 2023 mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana alitangaza juu ya maadhimisho ya  Siku ya Kwanza ya Watoto duniani kufanyika tarehe 25 na 26 Mei 2024. Siku ya Watoto (WMB), iliwakilishwa tarehe 2 Februari 2024, katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican. Ili kushiriki, unaweza kujiandikisha leo kwenye tovuti ya www.worldchildrenday.org.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari, Kardinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, chombo ambacho Papa alikabidhi jukumu la kuandaa Siku ya I ya  Mtoto Duniani, alikumbuka hali ya furaha iliyodhihirisha uteuzi huo, takriban miezi mitatu kabla ya siku hiyo ya watoto. “Ilionekana kama kutazama chemchemi ambayo ndege yake hai iliburudisha dunia na Kanisa kwa tumaini,na ndiyo sababu hamu ya Papa Francisko ni kwamba mkutano wa watoto wadogo na Papa uwe wakati ambao unakumbatia Kanisa kwa tarehe ya kawaida.

Nembo ya Siku ya Watoto Duniani
Nembo ya Siku ya Watoto Duniani

Siku ya Watoto duniani itaadhimishwa kwa ngazi ya dunia nzima Roma, mjini Vatican, ambapo wajumbe mbalimbali wa kitaifa watakutana, na katika ngazi ya kijimbo, na kuacha maandalizi kwa  Makanisa mahalia. “Tabia ya watoto inalipuka na ndio maoni mazuri na ya kupendeza, yaliyoandikwa kwa mwili, damu na roho, kwenye kifungu cha Ufunuo: “Tazama, nafanya vitu vyote kuwa vipya”, ambayo ndiyo mada iliyochaguliwa na Papa Francisko kwaajili ya  mkutano wa kwanza wa  mwezi Mei ijayo. Kuna jambo jipya katika Injili ambalo wavulana na wasichana wanalieleza kwa njia yao wenyewe aliwleza Kardinali hata hivyo mwenye  maikrofoni ya Radio Vatican - Vatican News alibainisha kuwa na ndicho ambacho Kanisa linataka kuweka katikati, kuonesha picha ya Kanisa ni mama, lakini pia linajua ni mtoto na ni mdogo. Watoto ni wapatanishi wakubwa wa furaha. Katika wakati wa huu wa kukengeuka, wa hali ya kukata tamaa ya kihistoria kama hii tunayoishi, watoto ni wabebaji wa imani thabiti katika ubinadamu.”

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa Utamaduni na Elimu, Siku ya Watoto Duniani ambayo inatoa uwezekano wa kuwa wahusika wakuu katika nyakati kali sana za usikivu, maombi na mafunzo ynaweza kuwa wakati wa uinjilishaji wa haraka, katika kukabiliana na kutojua kusoma na kuandika kwa vijana, watu na barubaru ambayo mwandishi wa habari alitaja. “Tunakabiliwa na shida ya maambukizi ambayo sio tu ya Kanisa lakini pia wa familia, shule, na siku hii ni mchango kwa maambukizi mazuri, yanayofaa kwa watoto”. Lakini Siku ya Pamoja na Watoto pia inaweza kuonwa kama mwito wa kuwaweka watoto katikati ya masilahi ya jamii na familia, kwa hivyo, mpango mzuri baada ya kesi za unyonyaji na unyanyasaji ambazo zimeibuka katika miongo ya hivi karibuni, iliyokumbukwa na mwandishi wa habari.

Nembo ya Siku ya Watoto Duniani
Nembo ya Siku ya Watoto Duniani

Mratibu wa Siku hiyo Padre Enzo Fortunato alitangaza uzinduzi wa meza ya kitaalamu ambayo pamoja na kamati ilianza kulifanyia kazi tukio hilo kwa kushirikisha taasisi mbalimbali, Majimbo na Vikariati ya Roma. “Jambo bora zaidi ni kuanza na watoto - alisisitiza - na ni nani zaidi ya watoto anayeweza kutufundisha kufanya hivi? Na ni ndoto gani kubwa kuliko amani? Wacha tuanze tena kutoka kwao, kutoka kwa urahisi na hamu yao ya siku zijazo. Wafransisko wa kidini walieleza kwamba njia tatu za maandalizi zitapendekezwa, moja ikihusishwa na kiroho, moja na mshikamano, moja na utamaduni, na uwezekano wa kuchagua moja ya mapendeleo ya mtu. Jijini Roma, Mei 25, saa 3 usiku, tutakutana mahali ambapo bado hatujatambulika kulingana na idadi ya waliojiandikisha. Mchana kutakuwa na muundo wa mkutano wa Novemba, unaozingatiwa kuwa toleo la “sifuri” la WMB, lenye shuhuda, wasanii, sauti za watoto na mazungumzo na Papa.  Tarehe 26 Mei 2024, saa 4.30 asubuhi, Misa katika Uwanja wa Mtakatifu  Petro itaadhimishwa na Papa Francisko. Maandalizi ya wimbo wa siku hiyo yamekabidhiwa kwa Monsinyo Marco Frisina, ambaye pia atashirikiana na kwaya za Zecchino d'Oro ambazo zitachangamsha mkesha. Kwa wale wanaotaka kushiriki katika Siku ya I ya  Watoto Duniani  tovuti maalum inatoa habari, inapendekeza malazi na inaonesha punguzo zinazotolewa kwa baadhi ya vyombo vya usafiri.

Marco Impagliazzo, rais wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, alitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa watoto kutoka maeneo ya vita na migogoro. “Tutajitolea kuwakaribisha, kwa namna fulani, watoto kutoka maeneo ya mwisho” alibainisha, , katika kujibu swali la mwandishi wa habari, kwamba kutakuwa na watoto wakimbizi nchini Italia, kutoka Eritrea, Siria, Afghanistan, na ambao walikwa watoto kutoka Haiti, Palestina, Ukraine, Sudan Kusini, Msumbiji, Nigeria na Colombia, pia wa imani nyingine za kidini. Na uwepo kwa kutapatana katika muktadha mzima wa maombi, alifafanua Kadinali Tolentino de Mendonça, katika kujibu swali lingine. “Tunaamini na kukiri imani yetu pamoja na waamini wengine, na hii ilikuwa dhahiri katika uzoefu wa Siku ya Vijana huko Lisbon, ambao pia ulikuwa na mipango ya kiekumene. “Tunapoomba sisi ni wa ulimwengu wote na watoto wataweka mfano mzuri” alisisitiza Kardinali.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, nembo ya Siku ya I ya Watoto Duniani pia iliwasilishwa, ambapo mchoro mdogo unaonesha wasifu wa Papa la Kanisa Kuu la  Mtakatifu Petro, na msalaba na taa ndani ambayo kuna alama za mikono za watoto wengi. Maana hiyo ilioneshwa na mtunzi  Marco Capasso: Papa linakumbatia, linakaribisha na linalinda watoto wadogo wanaowakilishwa na nyayo, ambazo rangi zao tofauti hukumbuka wingi wa tamaduni ambazo zinajumuishwa katika umoja unaokaribisha na kuthamini tofauti; taa ni mfano kwa Wakristo “wakichukuaji wa  taa”, wakati Msalaba unaashiria mateso na ufufuko wa Mwana wa Mungu, ambaye alifanyika mwanadamu kwa ajili yetu.”

Uwasilishaji wa Siku ya I ya Watoto duniani 25 na 26 Mei 2024
03 February 2024, 16:48