Tafuta

Kuanzia tarehe 4 -8 Machi 2024 mjini Vatican itafanyika kozi ya Toba ya wongofu wa ndani kwa mapadre waungamishaji pamoja na wanaojiandaa kuwa wahudumu wa Kanisa. Kuanzia tarehe 4 -8 Machi 2024 mjini Vatican itafanyika kozi ya Toba ya wongofu wa ndani kwa mapadre waungamishaji pamoja na wanaojiandaa kuwa wahudumu wa Kanisa.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Toleo la XXXIV la Kozi ya Toba ya Ndani Machi 4-8:utunzaji wa kichungaji wa sakramenti ya Upatanisho!

Idara ya Toba ya Kitume imeandaa Toleo la XXXI la Kozi ya Toba ya wongofu wa ndani kuanzia tarehe 4 -8 Machi 2024 mjini Vatican,Katika Basilika ya Mtakatifu Lorenzo karibu na Jumba la Kansela makao makuu ya Idara ya Toba ya Kitume.Leo hii kuliko wakati mwingine wowote,kiukweli,wahudumu wa huruma wanatakiwa kuwa na maandalizi ya kina na ya kisasa ya kitaalimungu,kiroho,kichungaji na kisheria.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Idara ya Toba ya Kitume (Penitenzieria Apostolica) imeandaa Kozi ya Toba ya wongofu wa ndani ambayo imefikia toleo la XXXIV kwa mwaka huu kuanzia tarehe 4-8 Machi 2024 mjini Vatican katika Basilika ya Mtakatifu Lorenzo, karibu na Jumba la Kansela ambayo ni makao makuu ya Idara ya Toba ya Kitume. Hii ni Kozi inayoandaliwa kila mwaka kwa ajili ya mapadre waungamishaji pamoja na wanaojiandaa kuwa wahudumu wa Kanisa.  Tukio hili la kila mwaka huandaliwa na kuhamasishwa na Idara ya Toba ya Kitume, kwa lengo la kuwapatia mapadre na watahiniwa wapya walio karibu na Daraja Takatifu fursa ya tafakari na mafunzo ya kina kuhusu Sakramenti ya Kitubio. Kozi hiyo inajumuisha uwezekano wa kushiriki ana kwa ana, na pia kwa mbali kupitia Mtandaoni. Uingiliaji kati uliopangwa utashughulikia, juu ya mtazamo wa fani nyingi na mada kuu zinazohusiana na toba la ndani na utunzaji wa kichungaji wa sakramenti ya Upatanisho. Leo hii kuliko wakati mwingine wowote, kiukweli, wahudumu wa huruma wanatakiwa kuwa na maandalizi ya kina na ya kisasa ya kitaalimungu, kiroho, kichungaji na kisheria. Hasa, hali za unyonge mkubwa na za kisasa zinazoathiri huduma ya toba zitashughulikiwa na kipaumbele kitatolewa kwa utatuzi wa kesi thabiti na ngumu ambazo zinakabiliwa na utambuzi na huruma ya Kanisa.

Ni muhimu kwa wahudumu wa upatanisho kujua jinsi ya kuwasaidia wanaokaribia sakramenti hiyo
Ni muhimu kwa wahudumu wa upatanisho kujua jinsi ya kuwasaidia wanaokaribia sakramenti hiyo

Watakaotoa kozi hiyo wanatabadilishana chini ya uongozi wa Kardinali Mauro Piacenza, Mhudumu mkuu pamoja na Monsinyo Krzysztof Jòzef Nykiel, Hakimu wa Idara ya Toba ya Kitume; Mons. Giuseppe Tonello na Mons. Giacomo Incitti, wote wakiwa ni Washauri na Wanasheria wa Idara ya Toba ya Kitume. Padre Fabio Rosini, Mkuu wa Ofisi ya Miito ya Jimbo la Roma, atazungumza juu ya uzoefu wake kama muungamishi, kubainisha aina fulani za watu waliotubu, wakati Padre Francesco Bamonte, ICMS, atashughulikia kesi za umiliki, akitoa viashiria kwa waamini jinsi ya kusaidia watu. Watu wengine wawili wa Idara ya Toba ya Ndani ya Kitume  watazungumza ni  Padre  Paolo Benanti TOR na Padre  Marco Panero SDB, ambao watazungumzia kuhusu Akili Mnemba na  juu ya utekelezaji wa huduma ya muungamishi. Hatimaye, itakuwa zamu ya maaskofu wawili wanaohudumu katika Curia Romana: Askofu Vittorio Francesco Viola, OFM, Katibu wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti, na Askofu Mkuu Rino Fisichella, Msimamizi Mkuu wa Baraza la Kipapa kwa Uinjilishaji, Sehemu ya masuala ya  kimsingi ya uinjilishaji ulimwenguni.

Huruma ya Mungu katika sakramenti ya kitubio
Huruma ya Mungu katika sakramenti ya kitubio

Awali Askofu Viola atakumbusha miongozo na dalili za kuadhimisha sakramenti, ambayo wakati mwingine ilipuuzwa kwa makosa, iliyomo katika Ibada ya Kitubio, wakati Askofu Mkuu Fisichella, kwa mtazamo wa kukaribia kwa ufunguzi wa Jubilei ya kawaida ya 2025, ataonesha maana na thamani ya Rehema kamili, ambayo kwa  kuitoa ni wajibu wa Idara ya Toba ya Kitume. Kozi hiyo itafuatiwa na mjadala, ambapo maswali ya ufafanuzi na maazimio yenye mashaka yatapendekezwa katika kesi madhubuti zitakazokusanywa kati ya watakaohudhuria. Washiriki wa Kozi hiyo watapokelewa kwa Mkutano na Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya Ijumaa tarehe 8 Machi 2024. Kozi itamalizika kwa Ibada ya Kitubio itakayoongozwa na Kardinali Mauro Piacenza, Mhudumu mkuu wa Idara ya Toba saa 10.30 jioni siku ya  Ijumaa tarehe 8 Machi, katika Kanisa la Roho Mtakatifu(Santo Spirito)huko Sassia, ambayo ni  Madhabahu ya Huruma ya Mungu.

Kozi ya Toba ya Ndani kuanzia 4 hadi 8 Machi 2024
29 February 2024, 16:34