Papa amekwenda Gemelli ya Kisiwa cha Tiberina kwa uchunguzi zaidi
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa uliyotolewa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Jumatano tarehe 28 Februari 2024 imebainisha kuwa: “Baada ya Katekesi yake, Papa Francisko alikwenda katika Hospitali ya ‘Isola Tiberina - Gemelli Isola’ kwa ajili ya vipimo vya uchunguzi. Mwishowe alirudi Vatican."”
Kama inavyojulikana, Papa Francisko amekuwa kwa siku hizi akiahirisha ratia za vikao vilivyokuwa vimepangwa kwa sababu ya afya yake. Kwa njia hiyo asubuhi ya tarehe 28 Februari 2024 pia, mwanzoni mwa katekesi yake kuu, aliwaeleza wamini na mahujaji waliohudhuria katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican kwamba: “bado yuko mafua kidogo” na kumuomba mmoja wa washirika wake, Monsinyo Filippo Ciampanelli, kusoma katekesi yake. Mara tu baada ya tukio hilo kwa hiyo, alikwenda kwenye ukaguzi katika hospitali ya Roma, iliyopo hatua chache kutoka mjini Vatican.