20224.02.14 Kukabidhiwa kwa Diploma za Kozi ya maandishi ya kiebrania katika Maktaba ya Kitume ya Vatican. 20224.02.14 Kukabidhiwa kwa Diploma za Kozi ya maandishi ya kiebrania katika Maktaba ya Kitume ya Vatican. 

Vatican,diploma zilizotolewa mwishoni mwa kozi ya hati za Kiebrania

Afla hiyo ilifanyika mnamo tarehe 13 Februari 2024 katika Maktaba ya Kitume ya Vatican.Hii ilikuwa ni safari ya kwanza ya aina hii iliyoundwa kutokana na mpango wa Papa.

Vatican News.

Wataalamu na wanasayansi 14 kutoka Marekani, Argentina, Israel, Kenya, Poland, Bulgaria, Costa Rica, Chile na Hungari walipokea diploma mwishoni mwa kozi maalumu iliyojikitia kwa ajili ya utafiti wa maandishi kwa mikono iliyotunzwa mjini Vatican. Kozi hiyo ilianza mnamo Julai mwaka 2023

Urafiki na ahadi ya pamoja

Padre Mauro Mantovani, Mwenyekiti wa Maktaba ya Vatican, alimpongeza mhusika mkuu wa maktaba, Monsinyo Angelo Vincenzo Zani kwa kuhitimisha kozi ya masomo. Alisisitiza kwamba utoaji wa diploma sio tu kitendo rasmi, lakini ishara ya urafiki na kujitolea kwa pamoja kwa utamaduni. Wakati huo huo, alionesha hamu yake ya kuendelea na safari hii katika siku zijazo. Akizungumza na Vatican News, alifafanua juu ya uzoefu huo ni “fursa nzuri ya kufahamiana zaidi, kukuza mazungumzo ya tamaduni na dini mbalimbali, yanayofungamana na maslahi ya pamoja kwa mtazamo wa kisayansi na utafiti, ambayo ni fursa nzuri ya kujenga madaraja na kuhamasisha  utamaduni wa mazungumzo.”

Ushuhuda a mazungumzo

Mmoja wa wataalamu waliotunukiwa diploma ni Mkuu wa Kiyahudi David Jason Fine kutoka Marekani. Akizungumza na Radio Vatican-Vatican News alisisitiza: “Hii ni ishara ya urafiki na mazungumzo ambayo tunaweza kuwa nayo kati ya dada zetu wawili wa kidini, ni ushuhuda wa ajabu wa wakati mzuri tuliomo na wa kazi nzuri ya Baba Mtakatifu Francisko.”

Mtandao wa mahusiano

Diploma hizo zilitunukiwa na Claudia Montuschi, mkurugenzi wa Idara ya Hati za Maktaba ya Kitume ya Vatican, ambaye alisisitiza jinsi makusanyo ambayo maktaba inatafiti kuhusu “mazungumzo haya kati ya tamaduni, dini, ustaarabu na hata lugha. Wakati huo huo akiakisi katika kila mpango wa kisayansi unaofanywa kati ya taasisi tofauti, pia kuna mtandao wa uhusiano na urafiki ambao unakua pamoja na mpango wa kisayansi.”

Kozi ya Kiebrania
15 February 2024, 16:02