Tafuta

Jengo la Baraza la Kipapa la Uinjilishaji (Propaganda Fide) Jengo la Baraza la Kipapa la Uinjilishaji (Propaganda Fide)  (Vatican Media)

Vatican:Kuanzia 19-23 inafanyika kozi ya wakurugenzi wa PMS wa lugha ya Kiingereza

Inafanyika kozi kwa wakurugenzi wanaozungumza Kiingereza wa Mashirika ya Utume wa Kipapa(PMS) kuanzia 19 hadi Ijumaa 23 Februari 2024 ikiongozwa na mada:Sasa na ya baadaye ya Missio ad gentes.Wajumbe wa kozi hiyo watatembelea hata Baraza la Kipapa la Uinjilishaji na maeneo yanayohusiana na Baraza hilo katika ratiba yao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuna wakurugenzi wapatao thelathini wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa (PMS)wengi wao kutoka Bara la Afrika wanaoshiriki mafunzo ya kimisionari yaliyofunguliwa tarehe tarehe 19 Februari 2024 mchana mjini Roma katika Kituo cha Kimataifa cha Uhuishaji wa Kimisionari (CIAM). Kozi hiyo iliyoandaliwa na Umoja wa Wamisionari wa Kipapa (PUM) inaratibiwa na Padre Dinh Anh Nguyen (OFM Conv,) katibu mkuu wa PUM, akisaidiwa na Padre Antony Chantry, Mkurugenzi wa Taifa POM Missio Uingereza & Wales na Mratibu wa Bara la Ulaya.

Siku ya Jumanne tarehe 20 Februari 2024  wajumbe wa Wakurugenzi wa Majimbo  wanaofuatilia kozi hiyo  iliyopangwa hadi Ijumaa tarehe 23 Februari  wametembelea Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji (Kitengo cha Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya mahalia). Kwa mujibu wa maelezo, yanabainisha kuwa “Siku tano inalenga kutoa maudhui ambayo yanaweza kuwa muhimu katika kazi ya uhuishaji, mafunzo na ushirikiano wa kimisionari. Programu inajumuisha kila asubuhi, baada ya adhimisho la Ekaristi na kusifu, kutembelea maeneo muhimu kwa historia na shughuli za Baraza la Kipapa la kimisionari na kwa ajili ya kazi ya kitume ya Kanisa.

Jumatano tarehe 21 Februari 2024,  wajumbe hao watashiriki Katekesi ya Baba Mtakatifu  Francisko na kutembelea Kanisa kuu la Mtakatifu Petro , siku ya Alhamisi tarehe 22 Februari  watafanya ziara ya Chuo cha Urbaniani ambacho ni Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana na kumbukumbu ya kihistoria ya Propaganda Fide imepangwa na siku ya Ijumaa  tarehe 23 ziara hiyo na katika  Chuo cha Mtakatifu Petro. Kinyume chake alasiri imetengwa  kwa ajili ya mikutano na vikao vya kazi vya kikundi. Kwa njia hiyo Alasiri ya Jumatatu tarehe 19 Februari, Katibu Mkuu wa PUM alianza kozi kwa hotuba ya makaribisho yenye lengo la kufupisha historia, utume na karama ya Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa.

Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana ilipokutana na Papa Francisko 21 Januari 2023
Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana ilipokutana na Papa Francisko 21 Januari 2023

Tarehe 20 na 21  Februari 2024 mikutano hiyo imekabidhiwa kwa Padre Tadeusz Nowak, Katibu mkuu wa Shirika la Kipapa la Kueneza Imani na Sr. Roberta Tremarelli, Katibu mkuu wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu  wa Kimissionari, akifuatiwa na tafakari ya Padre Antony Chantry kuhusu  siku zijazo za Missio ad gentes kutoka kwa mtazamo wa wale ambao wana mikono yao katika unga, iliyogawanywa katika siku mbili. Alhamisi 22 Februari alasiri, baada ya Mkutano na Padre Guy Bognon SSS, katibu mkuu wa Shirika la Kipapa la Mtakatifu Petro Mtume, hotuba inatarajiwa kutoka kwa Monsinyo Samuele Sangalli, katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji(kitengo cha kwanza) kuhusu maana ya utume leo hii na Huduma ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji. Anayefunga kozi hiyo atakuwa ni Padre Anh Nhue Nguyen na hotuba fupi kuhusu ujumbe wa Papa kwa Siku za Kimisionari Duniani za 2022, 2023 na 2024. Siku ya Ijumaa 23 Februari 2024 kozi itahitimishwa kwa hotuba ya katibu mkuu wa PUM ambayo itafuatiwa na kikao cha vikundi vya kazi na kulinganisha na hatimaye hitimisho.

20 February 2024, 15:38