Tafuta

2023.05.19 Banda la Vatican katika Maonesho ya katika sanaa ya Venezia 2023.05.19 Banda la Vatican katika Maonesho ya katika sanaa ya Venezia 

Venezia Biennale 2024:Banda la Vatican katika maonesho ya 60 Kimataifa ya Sanaa

Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu limehamasisha Banda kwenye Maonesho ya 60 Kimataifa ya Sanaa,ambapo mwaka 2024 yanaratibiwa na Adriano Pedrosa,akikita kwa mada ya: “Wageni kila mahali”kuhiana na haki za binadamu na waliotengwa.

Vatican News

Baraza la Kipapa la  Utamaduni na Elimu linashiriki katika kundaa Banda katika Maonesho ya 60 Kimataifa ya Sanaa ya ( La Biennale di Venezia), ambayo mwaka 2024 yatasimamiwa na Adriano Pedrosa, kwa kujikita na kauli mbiu ya “Mgeni kila mahali”. Banda hilo limejitolea kwa  ajili ya mada ya haki za binadamu na takwimu ya watu wali mwisho wa walimwengu, waliotengwa ambapo mara nyingi mitazamo yetu haiwafikii.

Katika maelezo kuhusu mada iliyochaguliwa wanabainisha kuwa: “Tunajaribu kuhimiza ujenzi wa utamaduni wa kukutana, ambao ni nguzo kuu ya Majisterio ya Papa Francisko. Kutokana na shauku hii huibua historia ambazo mara nyingi zinaweza kuonekana kuwa za kigeni kwetu, lakini ambazo kiukweli zinahusu kila mtu, kwa sababu zinasema juu ya njaa sawa ya upendo, shauku sawa ya maisha, upendo, kutokuwa na utulivu wa maana, kila kitu cha sanaa, daima kimekuwa kikitafuta kutafakari na kuwakilisha.

Kwa kushirikiana na Idara ya Utawala wa Magereza ya Wizara ya Sheria, kuanzia tarehe 20 Aprili hadi 24 Novemba 2024, katika Gereza la Wanawake la Giudecca, mradi wenye kaulimbiu: “Kwamacho yangu” utawasilishwa. Pendekezo la kisanii linachukua maneno ya Baba Mtakatifu, kwa hakika anapotuhimiza tutoke nje na kutazamana machoni ya wale tunaokutana nao, hasa waki wa mwisho, tukiwaalika wageni kuzingatia ukweli huo ambao mara nyingi huchukuliwa kuwa wa pembeni, na ambao mara nyingi huwa nje ya mjadala wa kiutamaduni.”

Kadinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu  amewateua Chiara Parisi na Bruno Racine kama wasimamizi wa Banda la Vatican. Na wasanii mashuhuri wa kimataifa: Maurizio Cattelan, Bintou Dembélé, Simone Fattal, Claire Fontaine, Sonia Gomes, Corita Kent, Marco Perego & Zoe Saldana, Claire Tabouret na, ushiriki maalum wa Hans Ulrich Obrist. Mkutano rasmi na waandishi wa habari wa kuwasilisha mradi huo umepangwa kwa siku chache za kwanza za mwezi Machi ujao  katika Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican.

09 February 2024, 10:12