Italia na Vatican wanaweza kufanya kazi pamoja kwa ajili ya amani
Vatican News
Utamaduni wa kipekee usio na uadui, lakini unaoshirikiana, kwa msingi wa maadili ya pamoja kulingana na uwajibikaji wa mahitaji ya kimwili na ya kiroho ya mtu huyo ndilo wazo lililojitikeza kwa miaka 40 baada ya kutiwa saini kwa marekebisho ya Mkataba, ambayo bado ni sura ya kumbukumbu kwa maendeleo ya amani ya uhusiano kati ya Serikali na Kanisa. Hayo yalisisitizwa tena na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, ambaye alizungumza Alhamisi 8 Februari 2024 katika mkutano uliohamasishwa na Mfuko wa Craxi katika Ukumbi wa Borromeo, nyumbani kwa Ubalozi wa Italia anaywakilisha Vatican ili kuadhimisha kumbukumbu ya kutiwa saini ya tarehe 18 Februari 1984 ya kile kinachoitwa “mikataba ya Villa Madama”, kuhusu marekebisho ya Mkataba wa 1929 ambao ulikuwa sehemu ya Makubalino ya Laterano.
Katika fursa hiyo Kardinali Parolin alielezea, juu ya kuchukua nafasi ya kufikiria juu ya matarajio ya siku zijazo. Awali ya yote alikumbuka matokeo mengi chanya ya taasisi ya ufadhili kupitia 8x1000, akisisitiza dhamira ya Kanisa kutumia pesa hizo kwa ajili ya mshikamano na kwa faida ya jumuiya ya kitaifa. Kusudi ni lile la dhana mpya ya uwajibikaji, kuchukuliwa kwa pande mbili pamoja na taifa la Italia, juu ya baadhi ya mambo, kuanzia amani jambo msingi na Vatican. Kardinali Parolin hasa alikumbuka vita vya Ukraine, Palestina na Israel, huku akisisitiza umuhimu wa dhamira ya pamoja ya suluhisho la haki na la kweli kwa mizozo hiyo.
Kadinali Parolin pia alisisitiza udharura wa kufanya kazi kwa wahamiaji na watu wasiojiweza zaidi. Uhamiaji ni jambo la kushughulikiwa kwa haraka, alisema, ambalo haliwezi kuondolewa au kudhibitiwa kwa kutoshirikishwa na hatua za sehemu, za kupunguza na kwa hivyo zisizofaa, lakini kushughulikiwa kwa kuhakikisha heshima ya utu wa mtu na mahitaji ya jamii za mahali hapo. Katika uwanja huu, na vilevile katika kukuza kazi, “kazi kati ya Kanisa na Serikali inaweza kusitawi kwa matokeo.
Kuhusu uhusiano kati ya Italia na Vatican ni wa kipekee katika ngazi ya kimataifa, ambapo alikumbusha Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Bwana Antonio Tajani, ambaye alizungumza juu ya Italia kama nchi isiyo ya kidini. Waziri Tajani alisisitiza usawa sawia uliohakikishwa na Kanisa, ambao hufanya mambo ambayo Serikali haiwezi kufanya. Mfano ulikwenda kwa Padre wa Nchi Takatifu, Padre Ibrahim Faltas na ukaribisho wake kwa watoto wanafika kutoka Gaza shukrani kwa meli ya Italia.
Wakati Jaji wa katiba Bi Antonella Sciarrone Alibrandi alikumbusha jinsi ambavyo Mkataba wa Laterano unavyoweza kuchukuliwa kuwa mfano wa mahusiano na maungamo mengine, wakati Seneta Stefania Craxi alikumbusha kwamba mikataba iliyotiwa saini na baba yake, aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo, ni mfano wa jinsi gani ya kukuza wingi wa kidini na ukweli wa dhati usio si wa maneno.