Askofu Carlassare:Sudan Kusini,Pasaka itupatie ujasiri wa kuchagua amani na udugu!
Na Massimiliano Menichetti
Picha za Dominika ya Matawi huko Rumbek zimeenea ulimwenguni kote ambapo Askofu wa jiji hilo alionekana akiwa amembeba mtoto begani, na idadi ya watu wanaoshangilia pande zote wakiwa na matawi mikononi. Katika mji muhimu zaidi wa Nchi ya Ziwa huko Sudan Kusini, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, Pasaka ni njia ya matumaini sio tu kwa Wakristo bali hata wasio. Papa alitembelea nchi hiyo ya Kiafrika, iliyokumbwa na ghasia na umaskini, mnamo mwezi Februari 2023, akitoa wito wa amani, haki na mshikamano. Katika mahojiano na Mwandishi wa Vatican News, Askofu Christian Carlassare, wa Rumbek, ameeleza kuwa "kuna ushiriki mkubwa katika Njia ya Msalaba ambayo hudumu asubuhi yote na huona uwepo waamini wengi na wasio wakatoliki."
Yafuatayo ni mahojiano kamili ya Askofu akielezea juu ya tukio la Juma Takatifu jimboni mwake
Linafanywa katika mitaa ya jiji na idadi kubwa ya watu na vijana wanaotunza vituo, na kufanya aina ya uwakilishi wa wahusika wa Mateso kutoka mwanzo hadi mwisho. Kwa hiyo, Yesu akiwa na msalaba na wahusika wengine wote wanaofungua msafara huo na kwenye vituo wanaonesha kile ambacho kinakaribia kutokea, huku wasomaji wakisoma vifungu vya Biblia. Na kweli watu wote, hata wasio Wakristo, wanashiriki uwakilishi huu kwa hisia kali, kiasi kwamba tunaona watu wakijipiga kifua na kulia na kulalamikia historia hii ya Yesu inayorudiwa katika maisha ya watu hawa. Kwa hiyo, sala ambayo pia ina nguvu kubwa ya ukombozi kwa sababu tunajitambulisha nayo na kuhisi jinsi mateso ya mtu mwenye haki yanavyoweza kuwapa matumaini watu wengine wengi. Na kisha, tutahitimisha kwa Mkesha na Misa ya Pasaka. Katika mkesha wa Pasaka, baraka ya moto ni nzuri sana kwa sababu kila wakati tunajaribu kubariki moto mpya, moto ambao haujatayarishwa hapo awali, lakini unaundwa wakati wa liturujia kwa njia ya jadi ya kusugua vijiti hadi kuanza kwa cheche za moto mpya. Na hivi ndivyo Mungu awezavyo kutufanyia: palipo na usiku huleta nuru, palipo na mauti huleta uzima mpya.
Picha za Dominika ya Matawi huko Rumbek zimeingia mioyoni mwa watu wengi: maandamano ambayo alimbeba mtoto mabegani mwake akiwa ameshika fimbo…
Ilikuwa ishara ya hiari. Katika Afrika wanapenda kuwakilisha uzoefu wa matukio, na si mara chache katika Dominika ya Matawi punda hutumiwa katika maandamano na kuhani anayepanda punda anawakilisha Kristo. Huko Rumbek, hata hivyo, hatuna punda kwa hivyo mwaka jana tulikuwa na maandamano rahisi kama tulivyozoea nchini Italia pia. Lakini zaidi ya wakati huu ninajisikia kuwa kama punda, aliyeitwa kwa huduma kubeba mizigo kama Yesu alivyoibeba yetu, kubeba nyuma ya mgongo wangu jimbo hili na watu wote wanaoumizwa, kutupwa au kudhihakiwa. Na hivyo wakati mtawa anayesimamia sacristy aliniambia kwamba punda hakupatikana nilimwambia: Usijali, nitajifanya punda. Na hivyo nikamchukua mtoto na kumpeleka kwenye Kanisa kuu.
Hakuna mtu aliyeshangazwa na ishara hii kwa sababu ndivyo inavyofanyika hapa, wakati mtu muhimu anafika kutembelea kijiji na hakuna njia nyingine ambayo ni zaidi ya kumwinua kwenye mabega yao na kumbeba. Hivi ndivyo wangefanya na Yesu, ikiwa mlango wa Yerusalemu ungekuwa hapa: wangemwinua, angalau wanafunzi, na kumleta hadi ndani ya mji. Na kwa hiyo kwa watu ilikuwa na thamani nzuri sana ya mfano: mvulana mdogo aliyebebwa mabegani ishara ya tumaini la jumuiya iliyopyaishwa.
Mnamo Februari 2023 Papa alikuja hija ya kiekumene. Alithibitisha katika imani, alizungumza juu ya amani na upatanisho. Ziara hii ilileta matunda gani?
Ninaamini kwamba matunda ya ziara ya Papa yalikuwa mengi sana na yalionekana hasa katika siku za ziara yake na katika miezi iliyofuata, lakini bado yanabaki kuwa ndani ya mioyo ya waamini na wengi wa wakazi wa Sudan Kusini leo. Ni wazi ishara hizo, ukweli huo ambao Papa aliomba sio maneno tu, bado yanabaki kuwa onyo wazi ambalo linaomba kujitolea kwa kila mtu. Kwa sababu hiyo, leo nadhani matunda muhimu ya ziara hiyo ni sisi wananchi wa Sudan Kusini, watu wenye mapenzi mema tuliosikiliza maneno ya Papa, tunaendelea kuombea amani na si kusali tu, bali zaidi ya yote kuikuza katika familia na jamii zao, kiasi cha kuambukiza nchi nzima ili amani ipatikane, licha ya yote. Na tunaweza kuliona hili, kwa sababu pamoja na dhuluma kubwa ambazo bado zinaendelea licha ya watu wengi kuhama makazi yao, licha ya msukosuko wa kiuchumi ambao watu maskini wanazidi kuwa maskini kwa maana ya kwamba thamani ya fedha ni ndogo kiasi kwamba hata kazi haina thamani tena, hakuna kitu na hivyo watu wanatatizika kupata huduma, huduma za afya, shule... Hapa, licha ya umaskini mwingi, watu bado hawakati tamaa na hawapendi vurugu au dhuluma, lakini kujaribu kuishi na kuishi kwa msingi wa mshikamano kati yao wenyewe. Nadhani idadi hii ya watu, iliyoungana na iliyojaa matumaini, ndiyo itaweza, siku moja, kuipa uhai nchi isiyoharibiwa na wenye uwezo, na wale walio na mamlaka, hasa ya silaha, au nguvu za kiuchumi, lakini nchi ambayo inatokana na mshikamano unaotokana na watu wanyenyekevu na rahisi.
Sudan Kusini ni nchi ambayo inakabiliwa na majeraha ya vita na umaskini, lakini kuna matumaini mengi. Je, unajiandaa vipi kwa ajili ya Pasaka na utafurahia vipi sherehe hii?
Kiukweli nilifurahishwa sana na ushiriki wa watu kwenye Sikukuu ya Matawi, hivi kwamba niliwauliza pia mapadre kwa nini sikuwahi kuona watu wengi sana katika Dominika. Pengine wanahisi kuguswa hasa na karibu na mateso ambayo Kristo aliteseka kwa ajili yetu na kwa hiyo wanataka kuhisi kuwa sehemu yake. kwa hivyo, katika Juma hili - Jumanne - pia tulikuwa na siku ya mafungo ya mapadre na watawa iliyohitimishwa na Baraza la Mapadre mahali ambapo tulipata ushirika. Jana (Jumatano)tulisherehekea Misa ya Krisma pamoja na mapadre wote na watu wengi kutoka jumuiya ya Wakristo, na niseme pia ilikuwa ni wakati wa muungano na furaha, shukrani kwa Bwana pamoja na ahadi zilizofanywa upya kwa Bwana ili kumtumikia katika ushirika. Pia tulipata muda wa kushiriki chakula cha mchana, tukiwapa mapadre muda wa kufikia parokia zao kwa ajili ya sherehe ya jioni ya leo: baadhi ya parokia, kiukweli, ziko mbali sana.
Je, Kanisa linachangia vipi katika mchakato wa ujenzi na upatanisho nchini?
Kanisa liko pamoja na watu wanaoteseka, linatia moyo, tumaini: si tumaini lisilo na maana bali uhakika kwamba Bwana yupo na anaandamana nao. Na aliyepondwa na kusulubiwa amefufuka na ndio mwanzo wa ufufuo wetu. Kwa hivyo, imani sio nyongeza, lakini ni zawadi muhimu kwa watu na kwa kila njia ya wokovu. Kwa hiyo Kanisa, katika kuhubiri na kuadhimisha, pia huongeza huduma ambayo inakuwa ni hatua muhimu ya kuinua, kuhamasisha na kuwafanya watu kuwa wahusika wakuu wa mabadiliko ya kibinadamu na kijamii. Hatuzungumzii tu juu ya upendo kwa maskini zaidi, kutoa huduma muhimu lakini pia kukuza shughuli za kiuchumi ili kuwafanya watu kuwa huru zaidi: pia tunafikiria miradi midogo ya kilimo ambayo tunajaribu kuiendeleza katika parokia zetu zote. Kufunza watu kwa maana ya kiraia, haki, amani; na tusisahau elimu katika shule za Kikatoliki, ambapo tunakuza malezi fungamani ya binadamu kwa kuthaminisha kila mtoto au mvulana au kijana aliye katika taasisi zetu. Na hii ni muhimu sana ambapo kijana badala yake anahisi kuachwa kando na labda kuendeshwa na masilahi ya wachache, kutafuta uwezekano wa kuelezea mali zao zote na ndoto zao zote kuelekea siku zijazo na kujaribu kuzifanikisha.
Nchi hiyo ina utajiri mkubwa wa mafuta lakini bado ni miongoni mwa maskini zaidi duniani. Je, ni hatua gani za kuchukua ili kuimarisha amani na kuwarudishia wananchi kile ambacho ni mali yao?
Haijahakikishiwa kwamba palipo na rasilimali pia kutakuwa na utajiri. Kwa bahati mbaya, wakati mwingi watu wanateseka zaidi na umaskini kutokana na mgawanyo mbaya wa mali. Sudan Kusini si maskini kwa sababu haina utajiri, bali kwa sababu haina amani. Vita vya Sudan vilizidisha mzozo wa kiuchumi kwa sababu serikali ya Sudan Kusini ilitegemea karibu kabisa unyonyaji wa mafuta: sasa bomba linalopitia Sudani limeharibiwa kwa kiasi na serikali ya Sudan haiwezi kutoa dhamana ya malipo hayo kwa Sudan Kusini ambayo ilitolewa hapo awali. Kwa hiyo pesa ya ndani inapoteza thamani kila siku ukilinganisha na dola, gharama za maisha ni kubwa sana sana na hakuna kuoanisha mishahara katika nchi ambayo kuna ukosefu wa kazi, na pale ambapo kuna uwezekano wa kufanya kazi, hata hivyo. inaonekana hakuna Ni muhimu kufanya kazi kwa sababu hupati kile unachohitaji ili kuishi.
Na hivyo watu hujikuta wakiishi siku hadi siku, hata wakiwa na uzoefu, wakitumia rasilimali hizo zinazoweza kupatikana. Ili kuimarisha amani - inaonekana kama kitendawili - amani inahitajika; mapambano dhidi ya uhalifu na rushwa - ambayo ni aina ya uhalifu - na kusaidia biashara na ujenzi wa uchumi ambao ni endelevu kuanzia hata shughuli ndogo za kiuchumi: kuanzia kilimo, mifugo, uvuvi... Sio tu unyonyaji wa rasilimali zinazotumika na kuliwa, bali pia kazi zinazozalisha rasilimali za aina nyingine. kupitia biashara yenyewe.
Je, ni maombi yapi na matashi yako kwa Pasaka hii nchini Sudan Kusini?
Shauku ya Pasaka: iwe kukutana na Kristo mfufuka, itukomboe kutoka kwa tamaa na woga, itupe ujasiri wa kufanya uchaguzi wa amani na udugu. Pasaka njema!