Askofu Mkuu Gallagher yupo Jordan kukutana na Mfalme na kutembelea Gaza
Kuanzia tarehe 11 hadi 14 Machi 2024,Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa yuko Nchi ya Mashariki ya Kati kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 30 ya Mahusiano ya Kidiplomasia.Katika ratiba yake ni pamoja na Misa Takatifu kwa Wakatoliki wa kawaida wa Nchi Takatifu,ziara katika maeneo ya Ubatizo wa Bwana,kukutana na Philippe Lazzarini Kamishna Mkuu wa (UNRWA).
11 March 2024, 11:21