Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Machi 2024 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Michel Jalakh, O.A.M. kuwa Askofu mkuu. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Machi 2024 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Michel Jalakh, O.A.M. kuwa Askofu mkuu. 

Askofu Mkuu Michel Jalakh, Katibu Mkuu Baraza La Kipapa La Makanisa ya Mashariki

Askofu mkuu mteule Michel Jalakh, alizaliwa tarehe 27 Agosti 1966 nchini Lebanon. Tarehe 15 Agosti 1983 akaweka nadhiri zake za kwanza kwenye Shirika la Antoni wa Maronite. Tarehe 21 Aprili 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kati ya Mwaka 2000 - 2008 alikuwa Afisa kwenye Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki. Kunako mwaka 2008 akajipatia Shahada ya Uzamivu; 15 Februari 2023 akateuliwa kuwa ni Katibu mkuu na 8 Machi 2024 Askofu mkuu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Machi 2024 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Michel Jalakh, O.A.M. kuwa Askofu mkuu. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Michel Jalakh, O.A.M. alizaliwa tarehe 27 Agosti 1966 huko Baouchrieh, nchini Lebanon. Baada ya malezi ya majiundo yake ya kitawa, tarehe 15 Agosti 1983 akaweka nadhiri zake za kwanza kwenye Shirika la Antoni wa Maronite “The Antonian Maronite Order” na hatimaye, tarehe 21 Aprili 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Kati ya Mwaka 2000 hadi Julai 2008 alikuwa Afisa kwenye Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki. Akajiendeleza kwa masomo ya juu zaidi na hivyo kunako mwaka 2008 akajipatia Shahada ya Uzamivu katika masuala ya Kanisa toka katika Taasisi ya Kipapa Kwa Ajili ya Makanisa ya Mashariki.

Maaskofu Kutoka Makanisa ya Mashariki Wakiwa kwenye Majiundo endelevu
Maaskofu Kutoka Makanisa ya Mashariki Wakiwa kwenye Majiundo endelevu

Tangu wakati huo akateuliwa kwenda kufundisha na hatimaye, kunako mwaka 2017 akateuliwa kuwa ni Gambera wa Chuo Kikuu cha Baabda kilichoko nchini Lebanon. Itakumbukwa kwamba, kati ya Mwaka 2013 hadi mwaka 2018 aliteuliwa kuwa ni Katibu wa Baraza la Makanisa Mashariki ya Kati. Tarehe 15 Februari 2023 akateuliwa kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki. Tarehe 8 Machi 2024 Baba Mtakatifu akampandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu na kwamba, tarehe 8 Juni 2024 atawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu, tayari kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu.

Uteuzi

 

13 March 2024, 13:30