Tafuta

Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya wanatoa wito kwa raia wote,hasa Wakatoliki,kujiandaa na kupiga kura katika uchaguzi ujao wa Ulaya wa Juni 2024. Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya wanatoa wito kwa raia wote,hasa Wakatoliki,kujiandaa na kupiga kura katika uchaguzi ujao wa Ulaya wa Juni 2024.  

COMECE:Katika uchaguzi wa EU,kuzeni maadili ya Kikristo na mpango wa Ulaya

Maaskofu wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya,wamesisitiza umuhimu wa kuunga mkono maadili ya jumuiya katika uchaguzi wa mwezi Juni ili kukabiliana vyema na changamoto za amani na uhamiaji,kukuza mshikamano,ulinzi ya maisha,familia na mazingira:upigaji kura kwa vyama vinavyopinga Ulaya na vyama vya watu wengi hauendani na dhamiri ya muumini,anayeitwa kutafuta faida ya wote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa kura ya kuwajibika kukuza maadili ya Kikristo na mpango wa Ulaya ndiyo msingi  tamko la Maaskofu wa Tume ya Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya (COMCE) kwa kuzingatia uchaguzi ujao wa Bunge la Ulaya  mwezi Juni wanawataka waamini wafanye chaguzi bora iwezekanavyo, wakichagua wanasiasa jasiri, wenye uwezo, wanaohamasishwa na maadili na ambao wanafuata wema wa wote. Ifatayo ni tamko kamili kutoka baraza hilo COMECE: “Sisi, maaskofu wanaowakilisha Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya tunatoa wito kwa raia wote, hasa Wakatoliki, kujiandaa na kupiga kura katika uchaguzi ujao wa Ulaya wa Juni 2024. Mpango wa Ulaya uliounganishwa kwa utofauti, wenye nguvu, wa kidemokrasia, huru, wa amani, wenye mafanikio na wa haki ni mpango tunaoshiriki na ambao tunahisi umiliki wake.

Viongo wa kidini wa Ulaya wanabinisha kuwa "Sote tumeitwa kueleza hili pia kwa kupiga kura zetu na kuchagua kwa kuwajibika Wabunge wa Bunge la Ulaya ambao watawakilisha maadili yetu na kufanya kazi kwa manufaa ya wote katika Bunge lijalo la Ulaya. Mpango wa ushirikiano wa Ulaya ulizaliwa kutokana na majivu ya vita vya kutisha vilivyoharibu bara letu katika karne iliyopita na kusababisha maumivu makubwa, vifo na uharibifu. Mpango huo uliundwa kwa nia ya kuhakikisha amani, uhuru na ustawi. Uliletwa kwa sababu ya ujasiri na mtazamo wa mbele wa watu ambao waliweza kushinda uadui wa kihistoria na kuunda kitu kipya ambacho kingefanya vita isiwezekane katika bara letu katika siku zijazo."

Maaskofu wa Comece wanafafanua kuwa "Mwanzoni, mpango huu ulikuwa mpango wa kiuchumi, lakini ulihusisha pia mwelekeo wa kijamii na kisiasa na maadili ya pamoja. Wengi wa waanzilishi wa Umoja wa Ulaya walikuwa Wakatoliki waliojitolea ambao walidumisha imani kubwa katika hadhi ya kila binadamu na umuhimu wa jumuiya. Tunaamini kwamba mpango huu, ulioanza zaidi ya miaka 70 iliyopita, lazima uungwe mkono na uendelezwe mbele. Leo Ulaya na Umoja wa Ulaya wanapitia nyakati zenye changamoto na zisizo na uhakika na mfululizo wa migogoro katika miaka ya hivi karibuni na masuala magumu ya kukabiliana nayo katika siku za usoni, kama vile vita vya Ulaya na katika vitongoji, uhamiaji na hifadhi, mabadiliko ya tabianchi, kukua kwa matumizi ya kidijitali na matumizi ya akili mnemba, jukumu jipya la Ulaya duniani, upanuzi wa Umoja wa Ulaya na mabadiliko katika Mikataba, nk. "

Tamko hili bado linaeleza kwamba "Ili kushughulikia maswala haya muhimu kwa kuzingatia maadili ya  msingi ya Jumuiya ya Ulaya na kujenga mustakabali bora kwa ajili yetu na vizazi vijavyo, sio tu barani Ulaya bali pia ulimwenguni, tunahitaji watunga sera wajasiri, wenye uwezo na wanaoongozwa na thamani ambao kwa uaminifu kwa  kufuata manufaa ya wote. Ni jukumu letu kufanya chaguo bora zaidi katika chaguzi zijazo. Kama Wakristo lazima tujaribu kupambanua vyema kwa ajili ya nani na kwa ajili ya chama gani cha kupiga kura katika wakati huu muhimu kwa mustakabali wa Umoja wa Ulaya. Hivyo hatuna budi kuzingatia mambo ambayo pia yanaweza kutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine - kwa mfano, uwezekano wa kuchagua wagombea au vyama pekee, programu za uchaguzi za vyama tofauti, wagombea wenyewe wanaojitokeza ..."

Viongozi hawa wa COMECA wanaeleza kuwa "Kuhusiana na mambo kama haya, Mabaraza ya Maaskofu katika kila nchi mwanachama yanaweza pia kutoa mielekeo muhimu. Zaidi ya hayo, lililo muhimu ni kwamba tupigie kura watu na vyama vinavyounga mkono kwa uwazi wa mpango wa Ulaya na ambao, tunafikiri ipasavyo, wataendeleza maadili yetu na wazo letu la Ulaya, kama vile kuheshimu na kukuza hadhi ya  kila binadamu, mshikamano, usawa, familia na utakatifu wa maisha, demokrasia, uhuru, usaidizi, utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja”…. Tunajua kwamba Umoja wa Ulaya si kamili na kwamba mapendekezo yake mengi ya kisera na kisheria hayapatani na maadili ya Kikristo na matarajio ya watu wake wengi, lakini tunaamini kwamba tumeitwa kuuchangia na kuuboresha kwa zana za kidemokrasia tunazozipata. Vijana wengi watapiga kura kwa mara ya kwanza katika chaguzi zijazo, baadhi yao wakiwa na umri wa miaka 16."

Maaskofu wa COMECE wanazidi kusema: "Tunawahimiza sana vijana kutumia kura yao katika uchaguzi ujao wa Ulaya na hivyo kujenga Ulaya ambayo inawahakikishia maisha yao ya baadaye na kutenda haki kwa matarajio yao ya kweli. Pia tunawatia moyo vijana Wakatoliki wa Ulaya wanaohisi wito wa kujihusisha na siasa kufuata wito huu, wakijitayarisha vyema kiakili na kimaadili ili kuchangia manufaa ya wote kwa moyo wa huduma kwa jamii. Katika hotuba iliyonukuliwa mara kwa mara iliyotolewa na Jacques Delors huko  Bruges, tarehe 17  Oktoba 1989 katika Chuo cha Ulaya, Rais wa wakati huo wa Tume ya Ulaya aliwahutubia wanafunzi vijana  kwa maneno yafuatayo: “Kwa maana mnaalikwa kutekeleza sehemu yenu katika kazi ya kipekee mpango  unaoleta watu na mataifa pamoja kwa bora, na si kwa ubaya zaidi.” Kama Maaskofu wa Ulaya, tunatoa wito huu kwa wanafunzi vijana wetu na kuuhutubia raia wote wa Ulaya. Hebu tushiriki katika mpango wa Ulaya, ambao ni mustakabali wetu, pia tupige kura kwa uangalifu katika chaguzi zijazo!"

Tamko liliidhinidhwa na wawakilishi wa COMECE:

Tamko hilo limeidhinidhwa na wajumbe wa Maaskofu wa COMECE: Askofu Mariano Crociata wa Latina (Italia), Rais,  Askofu Antoine Hérouard Mkuu wa Dijon (Ufaransa), Makamu rais Askofu Nuno Brás da Silva Martins wa Funchal (Ureno), Makamu wa Rais,  Askofu Czeslaw Kozon wa Copenhagen (Scandinavia) , Makamu wa Rais  Askofu Rimantas Norvila wa Vilkaviškis (Lithuania), Makamu wa Rais Askofu  Lode Aerts wa Bruges (Ubelgiji), Askofu  Virgil Bercea wa Oradea Mare (Romania). Askofu Msaidizi Joseph Galea-Curmi wa Malta,  Askofu Msaidizi Jozef Hal’ko wa Bratislava (Slovakia), Askofu Msaidizi  Theodorus C.M. wa Hoogenboom wa Utrecht (Uholanzi), Askofu Msaidizi Anton Jamnik wa Ljubljana (Slovenia), Askofu Philippe Jourdan Msimamizi wa Kitume wa Estonia, Askofu  Msaidizi Andris Kravalis wa Riga (Latvia)  Askofu Msaidizi Juan Antonio Martínez  wa Madrid  Juan Antonio Martínez Camino Camino Askofu Msaidizi wa Esztergom-Budapest (Hungaria), Askofu  Manuel Nin i Güell O.S.B. wa Kitume wa Ugiriki. Askofu Mkuu Kieran O'Reilly wa Cashel & Emly (Ireland), Askofu Franz-Josef Overbeck wa Essen (Ujerumani), Askofu  Christo Proykov wa Mtakatifu Yohane  XXIII wa Sofia (Bulgaria), Askofu Msaidizi Ivan Šaško wa Zagreb (Croatia)  Askofu Selim Selim Sfeir wa Maronites huko Cyprus,  Askofu Janusz Bogusław Stepnowski wa Łomża (Poland), Askofu Jan Vokál wa Hradec Králové (Jamhuri ya Czech), Askofu Msaidizi  Leo Wagener wa Luxemburg, Askofu  Aegidius Zsiisenstad (Austria).

Tamko la Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Ulaya kuhusiana na Uchaguzi wa Bunge la EU
14 March 2024, 16:44