Gallagher,Uturuki:Wanahitajika wakristo wa dhati katika vita ya tatu ya dunia
Vatican News
Safari ya Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, ilianza mnamo tarehe 28 Februari, hadi Uturuki katika hafla ya Jukwaa la Diplomasia la Antalya, mkutano wa kila mwaka wa diplomasia ya kimataifa ulioanza kufanyika Istanbul tangu 2021 na unaoleta pamoja watunga sera, wanadiplomasia na wasomi kubadilishana mawazo na maoni juu ya diplomasia, siasa na biashara.
Ziara ya Istanbul hadi Machi 2
Askofu mkuu Gallagahe kwa njia hiyo atakuwa yuko kati ya Mashariki na Magharibi hadi Machi 2, kama ilivyokuwa imetangazwa na akaunti kwenye X ya Sekretarieti ya Jimbo @TerzaLoggia ambayo ilichapisha maelezo juu ya mpango wa safari. Tarehe 29 Februari Alasiri Askofu Mkuu Gallagher aliongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu mjini Istanbul, iliyohudhuriwa na Patriaki Bartholomew I na ambaye pia alimpokea Askofu mkuu kwa ziara ya faragha.
Mnamo tarehe 2 Machi 2024, Askofu Mkuu Gallagher atashiriki katika kazi ya Jukwaa la Diplomasia. Hafla hiyo, iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, ambayo sasa iko katika toleo lake la tatu, tangu kuanza kwake, ambapo kwa kuongoza na kauli mbiu: “Kuendeleza Diplomasia katika Nyakati za Machafuko” tayari inafafanua nia ya kuchunguza njia za amani katikati ya machafuko duniani. Kupitia uingiliaji kati, meza za pande zote na fursa za mitandao, lengo ni kutafakari juu ya masuala muhimu ya sasa kama vile, ilivyoelezwa kwenye tovuti kwamba vita vinavyoendelea, ugaidi, uhamiaji, ongezeko la ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni, mabadiliko ya tabianchi na majanga na hatari zisizotarajiwa za Akili Mnemba
Kanisa, umoja katika utofauti
“Machafuko”, hasa, kama kichwa cha tukio kinavyosema, ambacho pia na juu ya Wakristo wote na imani yao wanaitwa kutoa mchango kwa ajili ya amani na manufaa ya wote”Askofu Mkuu Gallagher ndivyo alisisitiza katika mahubiri yake katika Kanisa Kuu, yaliyoadhimishwa kwa kuzingatia kumbukumbu ya miaka kumi na moja ya upapa wa Papa Francisko mnamo tarehe 13 Machi 2013.
Maadhimisho ya baraza la kwanza la kiekumene
Baadaye Askofu Mkuu alisema alivyofurahi kukutana na jumuiya ya Kikatoliki ya kile kinachojulikana kama “Nchi Takatifu ya Agano Jipya, mahali ambapo Mabaraza nane ya kwanza ya Kiekumene,na pia wachungaji na wawakilishi wa Makanisa mengine ya Kikristo ya Uturuki yalifanyika. Kwa njia hiyo mwaliko wa Askofu Mkuu Gallagher ulikuwa ni kwamba: “Wacha tuendelee pamoja, kama Wakristo, sote ni sehemu ya familia moja ya watoto wa Mungu na tuna imani sawa katika Kristo na Kanisa alilolianzisha.”
Askofu Mkuu aidha alifafanua “ukumbusho wa mwaka wa 1700 wa Baraza la Kiekumene la kwanza la Nikea kama tukio la kupendeza kuimarisha umoja wetu kama washiriki wa Kanisa la Kristo. Katika Baraza hilo, viongozi wa Kanisa walitangaza toleo la kwanza la Imani, ambalo baadaye lilikuja kuwa Imani ya Nikea-Konstantinopoli baada ya Baraza la pili la Kiekumene huko Konstantinople. Tunatumaini kwamba maadhimisho ya karibuni yataimarisha imani ya Wakristo wote." Lilikuwa tumaini la Katibu wa Mahusiano wa Vatican wa Mataifa.
Katika huduma ya wengine
Kutoka kwake pia alitoa mwaliko wa kutafuta mapenzi ya Mungu tu na kujiweka katika huduma ya wengine, kujifanya wadogo na kutoa maisha yetu kwa ajili ya wengine. Kiukweli, hii mara nyingi itasababisha unyonge na kushindwa mbele ya wengine, lakini Bwana ameonesha katika maisha yake mwenyewe kwamba njia hii inawezekana: “Hakuja kuwa bwana, lakini kuwa mtumishi,”alisema Gallagher. Kisha alihitimisha mahubiri yake kwa kukumbuka maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu hilohilo, wakati wa ziara yake huko Istanbul mnamo Novemba 2014: “Kanisa na Makanisa mengine na jumuiya za kikanisa zinaitwa kujiachilia kuongozwa na Roho Mtakatifu, na daima, kwa kubaki wazi, nyenyekevu na tiifu. Ndiye anayeleta maelewano kwa Kanisa.”