Tafuta

2024.03.25 Kazi mpya ya  Maupal kwa ajili ya Ujumbe wa Papa wa Kwaresima. 2024.03.25 Kazi mpya ya Maupal kwa ajili ya Ujumbe wa Papa wa Kwaresima. 

Imani,tumaini na upendo:kazi ya mwisho ya Maupal kuhusu Ujumbe wa Papa wa Kwaresima 2024

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu limechapisha kielelezo cha tano cha msanii maarufu wa mitaani,ambaye picha zake zilisindikiza maneno ya Ujumbe wa Papa Francisko katika safari ya Kwaresima 2024.

Vatican News

Papa ameshikilia mononi mwaka chombo cha kumwagilia maji huku akiweka maji kwenye mitungi mitatu ya mwisho ili kukuza mimea mitatu ambayo, kwenye lebo, imeandikwa majina ya fadhila za kitaalimungu:imani, tumaini na upendo. Nyuma ya Baba Mtakatifu Mtakatifu unaonekana umati wa watu wenye shangwe wa wanaume, wanawake, watoto, wazee, na wengine wakiwa wameshika mtungi au kopo la kumwagilia maji ili kumsindikiza Papa Fransisko katika utume huo. Ni kielelezo kipya cha msanii wa mtaani Maupal, yaani Mauro Pallotta, kilichotolewa na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu Jumatatu Kuu, tarehe 25 Machi 2024. Maonesho ya msanii huyo mashuhuri, na maarufu kwa michoro ya ukutani iliyowekwa wakfu kwa Papa katika mazingira ya Vatican, yalisindikiza Ujumbe wa Papa Francisko wa Kwaresima  2024 hadi  Siku Kuu ya Pasaka.

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu  kwa njia hiyo imetoa bango la tano na la mwisho kwenye mitandao yake ya kijamii, likiambatana na maneno kutoka kwa Papa ya waraka wake wa Kwaresima kwamba: “Ubinadamu wenye kuchanganyikiwa utahisi ubunifu mkubwa: mwanga wa tumaini jipya... Imani na upendo vinashikilia mkono wa msichana huyu mdogo wa matumaini.”

Ndugu msomaji katika Ujumbe wa  Baba Mtakstifu kwa ajili ya kipindi cha Kwaresima mwaka 2024, uliowasilishwa mnamo tarehe 1 Februari, uliongozwa na kauli mbiu: “Kupitia jangwa Mungu hutuongoza kwenye uhuru. Na umeongozwa na kifungu kutoka katika Kitabu cha Kutoka kisemacho: “Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka katika hali ya utumwa (Kut 20:1-17).”

Na uhuru kwa hiyo ndio imekuwa  mada kuu ya kazi  ya Maupal. Kutoka katika ujumbe wa  Kwaresima unatusaidia kujikomboa kutoka utumwani. Mungu anaunga mkono tumaini letu kwa njia ya kikanisa, jumuiya na safari ya kibinafsi ya uongofu ili kutuelekeza kuelekea nchi ambayo Yeye anataka kutupatia.” Taarifa ilibainisha kutoka katika Baraza la Kipapa ambalo linalongozwa na Kardinali Michael Czerny. Kwa njia hiyo kazi ya msanii Maupal imeoneshwa katika michoro mbali mbali tangu kuanza kwa Kipindi cha Kwaresima ambapo hatimaye tumefika majuma la matano.

Ndugu Msomaji tukirudi nyumba katika kazi ya kisanii, tarehe 18 Machi 2024 katika bango tulimwona Papa, akifuatwa na vijana wengine watatu, akiendesha baiskeli yake kuelekea barabara inayoonyesha"wema wa pamoja", kwa kuacha  nyuma njia ya "faida."

Kazi ya kisanii ya Maupal kuonesha barabara ya kufuata wema wa pamoja na kuacha njia za faida nyuma
Kazi ya kisanii ya Maupal kuonesha barabara ya kufuata wema wa pamoja na kuacha njia za faida nyuma

Katika kazi ya mchoro wa tarehe 11 Machi 2024 kutoka katika Ujumbe wa Kwaresima, ulionesha Papa akiwa ameshikana mikono na watoto wawili, mvulana na msichana wa rika na mataifa tofauti wakitembea na kucheza pamoja katika mzunguko.

Mchoro kuonesha vijana wa rika na mataifa tofauti wakicheza pamoja katika mzunguko
Mchoro kuonesha vijana wa rika na mataifa tofauti wakicheza pamoja katika mzunguko

Wakati huo huo mchoro wa tarehe 26 Februari 2024 wa msanii Maupal ulikuwa ni kilio cha wanaokandamizwa kutoka katika ujumbe wa Papa wa Kwaresima: "Hata leo kilio cha ndugu wengi wanaodhulumiwa kinafika mbinguni. Hebu tujiulize: je, kinatufikia sisi pia? Je, kinatutikisa? Je, kinatusonga?"

Mchoro ukionesha watoto wawili na Papa anaonesha kuwa kilio cha wanaokanamizwa kinafika hadi juu
Mchoro ukionesha watoto wawili na Papa anaonesha kuwa kilio cha wanaokanamizwa kinafika hadi juu

Mchoro mwingine  tarehe 19 Februari 2024 wa Maupal ulikuwa unahusu huru na chuki na hofu kutoka katika Ujumbe wa Papa: Papa akitazama nje kutokea kwenye pengo lililo wazi kando ya waya yenye ncha kali na kunyoosha mkono wake ili kusaidia mwanamume na mwanamke kutoroka kutoka katika gereza la "chuki" na "woga".

Papa akiwa kwenye nyaya za chuma ya miiba akitaka kuwakomboa wafungwa,
Papa akiwa kwenye nyaya za chuma ya miiba akitaka kuwakomboa wafungwa,

Tarehe Mosi Februari 2024 kwa hiyo kulikuwa na uwakilishi wa Ujumbe wa Kwaresima, ambapo kupitia Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo ya Kibinadamu alisema Ujumbe huo na kipindi cha Kwaresima ambacho kinaongozana na washiriki wake wote hadi kiini cha changamoto za wakati wetu. Mchoro wa Maupal ulionesha Kauli mbiu ya Ujumbe wa Kwaresima na wakati huo huo Papa akiwa na troli lenye kubeba gunia linaonesha neno:  Fede yaani Imani.

Msanii wa barabarani ambaye aliwakilisha kazi yake ya kisanii tarehe Mosi Februari kuhusu Ujumbe wa Kwaresima
Msanii wa barabarani ambaye aliwakilisha kazi yake ya kisanii tarehe Mosi Februari kuhusu Ujumbe wa Kwaresima

 

 

26 March 2024, 11:04