Kard.Parolin:kwa Papa,kujadiliana si kujisalimisha ni sharti la amani ya haki na ya kudumu
Vatican News
Tunachapisha maandishi kamili ya mahojiano yaliyofanywa kati ya Gian Guido Vecchi na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican iliyochapishwa 12 Machi 2024 ma Gazeti la ‘Corriere della Sera.’
Mwashamu inaonekana wazi kuwa Papa anaomba mazungumzo na sio kujisalimisha. Lakini kwa nini kuelekeza upande mmoja tu kati ya pande mbili, Ukraine na si Urussi? Na je, si kuibua “kushndwa” kwa walioshambuliwa kama motisha ya hatari ya mazungumzo kuwa kinyume?
“Kama ilivyokumbukwa na msemaji wa ofisi ya waandishi wa habari wa Vatican, akinukuu maneno ya Baba Mtakatifu ya tarehe 25 Februari iliyopita, wito wa Papa ni kwamba “masharti yaundwe kwa ajili ya suluhisho la kidiplomasia katika kutafuta amani ya haki na ya kudumu.” Kwa maana hii ni dhahiri kwamba uundaji wa masharti kama haya sio tu kwa upande mmoja, lakini kwa pande zote mbili, na sharti la kwanza kwangu linaonekana kuwa hasa la kukomesha uchokozi. Hatupaswi kamwe kusahau muktadha na, katika kesi hii, swali ambalo liliulizwa kwa Papa, ambaye, kwa kujibu, alizungumza juu ya mchakato wa mazungumzo na kwa namna ya pekee, juu ya ujasiri wa mazungumzo, ambayo sio kujisalimisha. Vatican inafuata barabara hii na inaendelea kuomba “kusitishwa kwa mapigano” na wavamizi wanapaswa kwanza kabisa kusitisha mapigano na kwa hivyo kufunguliwa kwa mazungumzo.” Baba Mtakatifu anaeleza kwamba, kufanya mazungumzo si udhaifu, bali ni nguvu. Sio kujisalimisha, lakini ni ujasiri. Na anatuambia kwamba lazima tuzingatie zaidi maisha ya mwanadamu, kwa mamia ya maelfu ya maisha ya wanadamu ambayo yametolewa dhabihu katika vita hivi katikati mwa Ulaya. Haya ni maneno ambayo yanahusu Ukraine na Ardhi Takatifu na migogoro mingine inayomwaga damu duniani.”
Je, bado kuna uwezekano wa kufikia suluhisho la kidiplomasia?
“Kwa kuwa haya ni maamuzi yanayotegemea utashi wa binadamu, daima kunabakia uwezekano wa kufikia suluhisho la kidiplomasia. Vita vilivyozuka dhidi ya Ukraine si athari za maafa ya asili yasiyoweza kudhibitiwa bali ya uhuru wa binadamu pekee, na utashi huo huo wa kibinadamu uliosababisha janga hili pia una uwezekano na wajibu wa kuchukua hatua za kukomesha hilo na kufungua njia ya suluhisho la kidiplomasia.”
Je, wasiwasi wa Vatican ni kuongezeka? Wewe mwenyewe ulizungumza juu yake, ukisema kwamba inatisha nadharia ya ushiriki wa nchi za Magharibi inatisha
“ Vatican ina wasiwasi juu ya hatari ya kuongezeka kwa vita. Kiwango cha kuongezeka kwa migogoro, mlipuko wa mapigano mapya ya silaha, mbio za silaha ni ishara za kushangaza na za kutatanisha kwa maana hii. Kupanuka kwa vita kunamaanisha mateso mapya, vifo vipya, waathirika wapya, uharibifu mpya, ambao huongezwa kwa wale ambao watu wa Kiukreni, hasa watoto, wanawake, wazee na raia, wanapata uzoefu katika miili yao wenyewe, wakilipa gharama kubwa ya hii ya vita visivyo vya haki.”
Francisko pia alizungumza juu ya mzozo wa Israel na Palestina, na kuibua “uwajibikaji wa washindani. Je, ni ni kitu gani kinafananishwa kwa hali hizi mbili?
“Hali hizi mbili kwa hakika zinafanana ukweli kwamba zimepanuka kwa hatari kupita kikomo chochote kinachokubalika, kwamba haziwezi kutatuliwa, kwamba zina athari katika nchi kadhaa, na kwamba haziwezi kupata suluhisho bila mazungumzo mazito. Nina wasiwasi juu ya chuki wanayozalisha. Je, ni lini majeraha makubwa ya kina kama haya yataweza kupona?”
Bado juu ya suala la kuongezeka: Papa amezungumza mara kadhaa juu ya hatari ya mzozo wa nyuklia, inatosha ajali moja,” je, hii ndiyo hofu msingi ya Vatican? “Ajali” kama ile ya huko Sarajevo mnamo 1914?
Hatari ya ajali mbaya ya nyuklia haikosekani. Inatosha kutazma tu utaratibu ambao wawakilishi fulani wa serikali wanatumia tishio hili. Ninaweza kutumaini tu kwamba hii ni propaganda ya kimkakati na sio “tishio” la tukio linalowezekana kweli. Kuhusu “hofu ya kimsingi ya Vatican, ninaamini kwamba wahusika mbali mbali katika hali hii ya kusikitisha wataishia kujifunga zaidi kwa masilahi yao wenyewe, bila kufanya wawezavyo kupata amani ya haki na utulivu.