Neno la Mungu kati ya watu maskini katika safari ya Pasaka kwenye nguzo za Mtakatifu Petro
Na Benedetta Capelli – Vatican
Kati ya vitanda vya kubahatisha, kwenye mabox ya makaratasi yatafutwayo na uchafu unaoweza kuonekana kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro pembeni nyakati za usiku, nguvu ya Ufufuko wa Yesu inafika hata hapo na ujumbe wake wa amani na matumaini usiomtenga mtu yeyote bali ambao unamwimarisha na kuhuisha mioyo wa wenye huzuni zaidi. Huo ni utume ambao watawa wa Klaretian wanautekeleza wakihuishwa na karama iliyochapishwa au kuanzishwa na mwanzilishi wa Shirika lao, Mtakatifu Antonio Maria Claret inayojikita katika shauku ya uinjilishaji na ujasiri wa kimisionari. Siku ya Jumanne tarehe 26 Machi 2024 iliwaona watawa hao katika toba na maskini kwa matazamio ya Siku Kuu ya Pasaka, Ufufuko wa Bwana.
Njia inayoongoza kwenye maombi ya pamoja
“Ili kufikia mpango huo ni muhimu kutazama hatua za nyuma.” Haya yalisemwa na Sista Elaine Lombardi, mmisionari wa Mtakatifu Anthony Maria Claret, ambaye alikumbuka jinsi miaka iliyopita katika parokia ya Torresina Roma, iliyowekwa wakfu kwa Mtakatifu Faustina Kowalska wa Huruma ya Mungu, baadhi ya vijana walianza safari muhimu kuanzia Tafakari ya Neno la Mungu (Lectio Divina) na kisha kukamilishwa na hamu kubwa ya kutaka kusaidia wengine na kwa hivyo na usambazaji wa chakula cha jioni kila siku ya Jumanne. “Tulianza chini ya Nguzo na novena ya Noeli na mwishoni watu wengi maskini wanaoishi huko walituomba tuendelee na mpango huo wa Tafakari na wasio na makazi mara moja kwa mwezi. Tunashiriki Neno la Mungu ambalo kiukweli hugeuka kuwa kushiriki maisha ya mtu, jambo kuu ni kwamba watalii wengi pia husimama na kuomba pamoja nasi,” alisisitiza Sr. Elaine.
“Siwezi kusoma Biblia…”
Kuna historia nzuri sana ambazo tumekusanya” alisema Sr Eliane kwa hisia. “Mmoja wao, Francis, ambaye ana historia fulani ya maisha na anaishi mitaani, alianza kushiriki katika Tafakari ya Neno la Mungu na alikuwa na huzuni kutokana na matatizo ambayo alikuwa akikutana nayo kila siku. Siku moja, mwisho wa maombi, alinikaribia kuniomba Biblia na nikampatia ile niliyokuwa nayo mkononi na tuliyoitumia kwa ajili ya Tafakari hiyo, iliwekwa kwenye madhabahu ndogo tunayotengeneza kwa kutumia moja ya vitabu hivyo, masanduku ya maskini na mavazi tunayobeba. Aliipokea lakini Juma lililofuata akaja kuzungumza nami ili kuniambia kuwa hajui kusoma.” Fransis alipata mtu anayemfikiria, anayemsikiliza na ambaye anaingia naye katika uhusiano na kwa sababu hiyo hakusita kumwambia mtawa huyo kwamba nyakati za maombi alizopitia na Neno la Mungu limefanya shauku ya kutaka kujua Injili na kwa hiyo kujifunza kukua ndani yake na kusoma. “Tulichukua hatua mara moja na kutafuta mahali ambapo angeweza kukuza hamu yake hii. Nadhani hii ni nzuri sana na imenigusa sana.