Papa ameteua katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na vyama vya Kitume,Padre Aitor Jiménez Echave. Papa ameteua katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na vyama vya Kitume,Padre Aitor Jiménez Echave.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Padre Echave katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na vyama vya Kitume

Machi Mosi 2024,Padre Aitor Jiménez Echave ameteuliwa kuwa katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na vyama vya Kitume.

Vatican News

Alhamisi tarehe 29 Februria 2024 Baba Mtakatifu Francisko alimteua Padre Aitor Jiménez Echave, kuwa katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Maisha ya Kitawa  na Vyama vya Kitume ambapo  hadi uteuzi huo alikuwa ni afisa wa taasisi hiyo hiyo.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatican imeripoti kuwa  Monsinyo Jiménez Echave alizaliwa tarehe 29 Desemba 1962 huko Luchana-Baracaldo (Hispania). Tarehe 13 Septemba 1987 alifunga nadhiri za daima katika Shirika la Wamisionari wa Moyo Safi wa Maria na tarehe 30 Aprili 1989 akapata daraja la Upadre.

Majiundo yake alipata Shahada ya Uzamivu katika Sheria ya Haki kwa pande zote mbili na Shahada ya Uzamivu ya Taalimungu ya Maisha ya Wakfu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano jijini Roma. Ana diploma kadhaa, ikiwa ni pamoja na moja ya Sheria ya Kanuni ya Mashariki. Tangu mwaka 2006 amekuwa afisa wa Baraza hilo la Kipapa hadi kuchaguliwa kwake.

 

01 March 2024, 16:37