Papa akutana na Kamati ya maandalizi ya Siku ya Watoto duniani
Vatican News
Kwa mujibu wa taarfa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari mjini Vatican kwa waandishi ni kwamba: “Leo mchana saa 9:00 alasiri katika Nyumba ya Mtakatifu Marta, mjini Vatican Baba Mtakatifu Francisko amepokea Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Wtoto Duniani, pamoja na hafla ya kuchapishwa kwa ujumbe wake kwa ajili ya tukio hilo.”
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican kwa waandishi wa habari inabainisha kuwa “akiwasalimu waliohudhuria, Papa alitoa baadhi ya maneno ya shukrani kwao, akishangaa juu ya mateso ya watoto, hata katika hali ya migogoro, juu ya unyonyaji wao, na akitumaini kwamba Siku hiyo inaashiria "kuinua ufahamu" kwa maana hiyo pana.”
Kamati hiyo iliongozwa na Mratibu, Padre Enzo Fortunato, na Monsinyo Cesare Pagazzi, Katibu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, na waliokuwepo Katibu Mratibu wa Kamati hiyo, Aldo Cagnoli, na wawakilishi wa baadhi ya vyombo vinavyohusika zaidi vya maandalizi kama vile Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Ushirika wa Auxilium,Shirikisho la Soka la Italia, pamoja na Mkuu wa Ujumbe wa Timu ya Taifa ya Italia, viongozi wa Michezo na Afya, wajumbe wa Manispaa ya Roma, Mkoa wa Lazio, Kundi la Reli ya Taifa(FS) na taasisi mbalimbali zinazopenda kuandaa Siku hiyoMkutano huo baadaye ulihitimishwa mara.