Papa akutana na Rais wa Jamhuri ya Seychelles
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumamosi, 16 Machi 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekutana katika Jumba la Kitume Vatican na Rais wa Jamhuri ya Seychelles, Bwana Wavel Ramkalawan, ambaye mara baada ya mkutano huo pia Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mhusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican inabainisha kuwa wakati wa mazungumzo yao na Sekretarieti wameonesha kwa uhai wote pongezi za mahusiano mema yaliyopo uzote mbili kati ya Vatican na Jamhuri ya watu wa Seychelles, ambapo ni pamoja na mchango wa Kanisa Katoliki katika Huduma kwa jamii hasa, katika mantiki ya utunzaji na Elimu.
Hatimaye, katika mazungumzo hayo wamebadilishana mitazamo juu ya hali ya kijamii na kisiasa katika Nchi. Kwa kusisitiza kwa namna ya pekee mada muhimu za pamoja, miongoni ni ulinzi wa watoto na mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya, na vile vile kuzungumzia juu ya hali za kimataifa.
Katika ziara hiyo rais alifika mjini Vatican kuanza mkutano saa 2.25 hadi 2.40 na kuondoka karibu saa 2.50 asubuhi. Lakini pamoja na hayo hawakukosa kubadilishana zawadi ambapo Baba Mtakatifu amemzawadia Rais, Sanamu ya shaba, yenye kauli mbiu: “Utunzaji wa Uumbaji”; Hati za kipapa; Ujumbe wa Amani wa 2024; kitabu cha Njia ya Msalaba(Statio Orbis cha tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na Nyumba ya Vita Vatican ( LEV); na hatimaye kitabu cha Nyumba ya Kipapa chenye katekesi , kilichohaririwa na Mkuu wa Nyumba ya Kipapa.
Kwa upande wa Rais wa Seychelles: Mchono wa shaba wa Kombe kwenye mchanga; Muanzi wa Jadi uliochorwa picha ya Bikira Maria.