Papa amekutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Kansela wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Olaf Scholz, Jumamosi tarehe 2 Machi 2024 katika Jumba la Kitume. Baadaye, Scholz, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican ilivyoarifu, “alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akifuatana na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu Msaidizi wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.”
Wakati wa mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican, wameonesha kuridhika kwa uhusiano mzuri na ushirikiano wenye manufaa uliopo kati ya Vatican na Ujerumani, huku wakionesha umuhimu wa imani ya Kikristo katika jamii ya Ujerumani. Kisha waliakisi "baadhi ya masuala ya maslahi ya pamoja, kama vile hali ya uhamiaji na marejeo maalum yalitolewa kuhusu migogoro ya Ukraine na Israeli na Palestina, na dhamira iliyofuata ya amani, katika kutafuta bila kuchoka suluhisho la kidiplomasia ambayo itawezesha kusitishwa kwa uhasama haraka iwezekanavyo.”
Wakati wa ubadilishanaji wa zawadi za kiutamaduni, Scholz alimpatia Papa mpira rasmi wa Kombe la Ulaya 2024 (UEFA EURO 2024) na sanamu ya udogo ya dubu na nembo ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.
Na kutoka kwa Baba Mtakatifu alimpatia, kazi ya shaba yenye kichwa “Upendo wa Kijami”, inayoonesha mtoto akimsaidia mwingine kuamka, na imeandikwa: “Msaada wa Upendo;” aidha wingi wa hati za upapa; Ujumbe wa Amani wa mwaka huu 2024; kitabu Njia ya Msalaba(Statio Orbis ya 27 Machi 2020), kilichohaririwa na LEV.