Papa amemteua Balozi wa Vatican nchini Papua Guinea Mpya
Vatican News
Ijumaa tarehe Mosi Machi 2024, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi wa Vatican nchini PapuaGuinea mpya Monsinyo Mauro Lalli, aliyekuwa Mshauri wa Ubalozi kwa kumwinua moja kwa moja hadhi ya Uskofu Mkuu kuwa na kupewa makao ya Pausula.
Wasifu wake
Monsinyo Mauro Lalli alizaliwa huko Atessa (Chieti) nchini Italia mnamo tarehe 17 Septemba 1965. Alipewa daraja takatifu la upadre baada ya majiundo yake mnamo tarehe 14 Julai 1990, kwa ajili ya Jimbo katoliki la Chieti – Vasto, Italia.
Ana shahada ya Sheria ya Haki kwa pande zote mbili. Alijiunga katika Huduma ya Diplomasia ya Vatican mnamo tarehe 1 Julai 1999, baadaye kuendelea na shughuli katika uwakilishi wa Ubalozi wa Kipapa nchini Guatemala, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Msumbiji, Romania, Kroazia, India, Iraq, Yordan na Cyprus. Lugha anazofahamu ni Kiingereza, kifarasnsa, Kireno na Kihispania.