Tafuta

2024.03.11 Balozi wa mpya wa  Vatican Nchini Italia na Jamhuri ya San Marino ni Askofu Mkuu Petar Antun Rajič. 2024.03.11 Balozi wa mpya wa Vatican Nchini Italia na Jamhuri ya San Marino ni Askofu Mkuu Petar Antun Rajič. 

Papa amemteua Balozi wa Vatican Nchini Italia Mons.Petar Rajič

Papa amemteua Balozi wa Vatican Nchini Italia na Jamhuri ya San Marino,aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini Lithuania,Latvia na Estonia. Na Rais wa CEI amemkaribisha Balozi Mpya na kumuaga aliyetangulia kuhudumu kwa miaka 7.

Vatican News

Jumatatu tarehe 11 Machi 2024, Baba Mtakatifu Francisko amemteuta Balozi wa Vatican Nchini Italia Askofu Mkuu Petar Rajič. Hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Lithuania, Latvia na Estonia.

Shukrani kutoka kwa Rais wa CEI

“Tunamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa umakini wake endelevu na wa kudumu kuelekea Makanisa nchini Italia. Uteuzi wa Balozi wa  kitume ni kielelezo cha dhamana ya pekee ya ushirika ambayo inafanywa upya kati ya Kiti cha Kitume na Jumuiya za Kikanisa.”  Ndivyo Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) amethibitisha kufuatia uteuzi wa Askofu Mkuu  Petar Rajič kama balozi wa Vatican  nchini Italia na Jamhuri ya San Marino.

Shukrani kwa Balozi aliyetangulia Kardinali Tscherring

“Kwa wakati huu tunapenda kutoa shukrani zetu kwa Kardinali Emil Paul Tscherrig kwa huduma ambayo ameifanya, katika miaka hii saba, kwa ajili ya Makanisa yetu." Amesisitiza Rais wa Cei na kuongeza: "Imekuwa wakati mkali, unaojulikana na mabadiliko makubwa ambayo yanaathiri maeneo na pia yaliyoathiriwa na janga. Kiukweli tulipata fursa ya kuona matendo na ushauri wake wa thamani katika kufanya vifungo vya umoja na Vatican kuzidi kuwa thabiti na kufaa na katika kujenga uhusiano na Mamlaka za Serikali.” Amesisitiza Rais wa CEI lakini pia “Kwa hisia kama hizo tunamkaribisha Askofu Mkuu Petar Rajič leo, tukimshukuru kuanzia sasa na kuendelea kwa huduma atakayoifanya miongoni mwetu.” Anahitimisha.

11 March 2024, 15:02