Papa ameridhia kutangazwa Makuhani na watawa 15 waliouawa wakati wa Vita ya II ya Kidunia
Vatican News
Miongoni mwa watakaotangazwa kuwa Wenyeheri hivi karibuni ni wafiadini 16, waliouawa kwa chuki kutokana na imani chini ya Unazi na ukomunisti wa Kisovieti. Kikundi hicho kinajumuisha Padre aliyepigwa risasi Ujerumani ya kinazi na watawa 15 wa asili ya Ujerumani waliouawa na askari wa Jeshi lekundu au waliokufa katika kambi za mateso katika Urussi ya kisoviet. Haya yalijiri katika mkutano wa Baba Mtakatifu Francisko na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Wenyeheri na Watakatifu, Siku ya Alhamisi, tarehe 14 Machi 2024 na kuidhinisha kutangazwa kwa kanuni zinazohusiana na wanawake na wanaume 25 wa Kikatoliki.
Idhinisho hilo ni pamoja na kutambuliwa kwa mauaji ya shahidi wa wanawake 15 watawa wazaliwa wa Ujerumani ambao walikuwa wakihudumu nchini Poland wakati wa uvamizi wa Jeshi Jekundu: Sr. Christophora Klomfass na wenzake 14 wa Shirika la Masista wa Mtakatifu Catherine, Bikira na Mfiadini (CSC) walifariki mwaka 1945. Watawa hao waliuawa kwa sababu ya chuki kwa imani na askari wa kisovieti, wakivumilia kubakwa, kuteswa, na kifo kutokana na magumu, kutendewa vibaya, au magonjwa katika kambi za mateso katika Urussi ya kisovieti. Kama ishara kali ya dharau kwa imani ya Kikristo, watesaji wao mara nyingi walikata na kurarua mavazi yao ya kitawa.
Padre wa amani na uekumene wakati wa Hitler
Padre Max Josef Metzger, wa jimbo la Ujerumani na mwanzilishi wa Taasisi ya Kidunia ya Societas Christi Regis, aliuawa mnamo tarehe 17 Aprili 1944, huko Ujerumani ya kinazi. Padre alikuwa mtendaji katika harakati za kupinga amani na kiekumene, na mnamo 1917 alianzisha Ligi ya Amani ya Ulimwengu ya Msalaba Mweupe. Miaka kumi baadaye, alishiriki kama mwangalizi wa Kikatoliki kwenye Bunge la Lausanne, ambalo lilitokeza Baraza la Kiekumene la Makanisa. Baada ya kuibuka kwa Unazi, alizungumza waziwazi dhidi ya Hitler. Alikamatwa kwa mara ya kwanza mnamo 1939 na mara ya pili mnamo 1943. Akiwa amehukumiwa kifo, alipigwa risasi tarehe 17 Aprili 1944, katika gereza la Brandenburg-Görden. Alijua kwamba kujitolea kwake kwa amani na uekumene, na vilevile kukataa kwake utawala wa kinazi katika jina la Kristo, kungemgharimu uhai wake.
Wengine watakaotangazwa wenyeheri
Papa Francisko pia alitambua miujiza inayohusishwa na maombezi ya Watumishi wa Mungu watatu, ili wa watagazwe kuwa wenyeheri. Miongoni mwa hao ni Patriaki wa Antiokia wa Wamaroni, Stephane Douayhy, Mlebanon, aliyeishi katika karne ya 17 (1630-1704). Alifanya kazi kubwa ya kusaidia maskini na kwa ajili ya mazungumzo ya kiekumene kati ya Mashariki na Magharibi. Papa pia alisafisha njia ya kutangazwa Mwenyeheri José Torres Padilla, padre wa jimbo la Hispania, mwanzilishi mwenza wa Shirika la Masista wa Shirika la Msalaba (1811-1878), na Camillo Costa de Beauregard, Mfaransa, kuhani wa jimbo (1841-1910), walimpatia jina la utani baba wa yatima kwa kuanzisha kituo cha watoto yatima cha Le Bocage huko Chambery.
Wenyeheri wapya ni: - Geervaghese Thomas Panickaruveetil Mar Ivanos, Askofu Mkuu wa Trivandrum wa Kanisa Katoliki la Syro-Malankara, mwanzilishi wa Shirika la Kumwiga Kristo mwaka 1919 Bethany Ashram na Masista wa Kumwiga Kristo Bethany Madhom, mwanzilishi wa uekumene nchini India na askofu wa kwanza wa Kanisa Katoliki la Syro-Malankara;
- Mbrazil Padre Liberio Rodrigues Moreira, (1884-1980) ambaye alitumia maisha yake kwa ajili ya wagonjwa na maskini na kuishi na roho ya kina ya Kikristo majaribu ya maisha, mwabudu wa Ekaristi bila kuchoka;
- Mlei aliyejulikana Antonio Tomičić, (1901-1981) Mkroatia wa Shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchin,(OFMcap) ambaye wakati wa miaka ya ukomunisti, wakati wa kuvaa ishara za kidini hadharani alichochea kejeli na uadui, hakuwahi kuacha tabia yake, akivumilia matusi ya umma na kudumu, akiwa na tumaini thabiti katika Bwana, katika kutafuta kwake mahitaji ya akina ndugu;
- Mlei wa Kiitaliano na mama Maddalena Frescobaldi Capponi, (1771-1839) mwanzilishi wa Shirika la Masista wa Passionist wa Mtakatifu Paulo wa Msalaba;
- Maria Alfinda Hawthorne, (1851-1926) mwanzilishi wa Masista wa Dominika wa Mtakatifu Rose wa Lima, aliyezaliwa katikati ya karne ya 19 katika familia ya Kiprotestanti katika jimbo la Massachusetts huko Marekani na akawa Mkatoliki huko Ulaya pamoja na mumewe, ambaye kutoka kwao alijitenga kwa sababu ya ulevi wake, kisha akajitolea kwa huduma ya Kristo kwa wagonjwa wa saratani;
- Angelina Pirini, (1922-1940) kiongozi mlei wa Parokia ya Matendo ya kikatoliki huko Cesenatico mkoa wa Emilia Romagna Italia, alikufa mwaka 1940;
- Elisabetta Jacobucci, (1858-1939) anayejiita dada wa Taasisi ya Alcantarine. Mfansiskani wa msekulari, aliyeishi mwanzoni mwa karne ya 19 na 20. Daima alikuwa tayari kukubali kazi za unyenyekevu zaidi, na aliweza kuchanganya kipengele cha kujinyima cha kutafakari Mateso na utume mkali wa hisani kwa yatima na wazee.