Papa amewateua Makatibu wawili wasaidizi wa Baraza la Kipapa la Makleri
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 12 Machi 2024, amewateu makatibu wawili wasaidizi kwa ajili ya Ofisi ya Baraza la Kipapa la Makleri, Mheshimiwa Padre Enrico Massignani, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Kansela wa Jimbo la Vicenza (Italia);na Monsinyo Eamonn McLaughlin, ambaye hadi uteuzi alikuwa Afisa wa ofisi hiyo.
Wasifu wake
Padre Massignani alizaliwa tarehe 2 Februari 1976 huko Valdagno (Italia) na kupewa daraja la Upadre tarehe 7 Juni 2003 kwa ajili ya Jimbo la Vicenza. Katika mafunzo yake ana shahada ya Sheria za Kanoni kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoariana Roma. Ameshikilia nafasi mbali mbali katika jimbo miongoni mwake ni Kansela; Hakimu wa Mahakama ya Kikanisa ya Kanda yaTriveneto; Msimamizi wa Parokia ya Mtakatifu Cristofor huko Tonezza ya Cimone.
Na katibu mwingine wa pili Papa amemtesuia msaidizi katika Ofisi hiyo ni Monsinyo Eamonn McLaughlin, ambaye hadi uteuzi alikuwa katika Taasisi hiyo ya Curia.
Wasifu
Monsinyo McLaughlin: alizaliwa tarehe 21 Juni 1977 katika Wilaya ya Donegal (Ireland) na alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 30 Juni 2002 kwa ajili ya Jimbo la Raphoe. Alipata leseni katika taalimungu katika Taasisi ya Yohane Paulo II, jijini Roma, Italia. Alifunika nyadhifa mbalimbali ambamo miongoni mwake ni Mjumbe wa Baraza la Mapadre na Mkurugenzi wa Mahakama ya Ndoa. Tangu 2017 amekuwa afisa wa Baraza la Kipapa la Wakleri.