Papa Francisko amekuwa akisema waziwazi kuwa "kufanya mazungumzo kamwe siyo  suala la kujisalimisha." Papa Francisko amekuwa akisema waziwazi kuwa "kufanya mazungumzo kamwe siyo suala la kujisalimisha." 

Papa Francisko anaomba Ukraine iwe na ujasiri wa majadiliano

Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican,Dk.Bruni akiwajibu waandishi wa habari kuhusiana na kauli ya Baba Mtakatifu katika mahojiano na Radio na Televisheni ya Uswisi (RSI):“Papa anatumia sura ya bendera nyeupe iliyopendekezwa na mhoji ili kuonesha kusitishwa uhasama,mapatano yafikiwe kwa ujasiri wa mazungumzo.Matumaini yake ni suluhisho la kidiplomasia kwa ajili ya amani ya haki na ya kudumu.”

Vatican News

Kupitia Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Dk. Matteo Bruni akijibu maswali ya waandishi wa Habari kuhusiana na kauli ya Baba Mtakatifu katika mahojiano  ya hivi karibuni na Radio na Televisheni ya Uswisi (RSI): “Papa alitumia neno la Bendera nyeupe akijibu huku akichukua sura iliyopendekezwa na aliyekuwa akimuoji, ili kuashiria kusitishwa kwa uhasama, mapatano hayo yafikiwe kwa ujasiri wa mazungumzo. Na matumaini yake ni suluhisho la kidiplomasia kwa ajili ya amani ya haki na ya kudumu.”

Hata hivyo mahali pengine katika mahojiano, akizungumzia hali nyingine ya mzozo, na hasa akizungumzia kila hali ya vita, Papa alisema waziwazi kuwa: “mazungumzo kamwe siyo kujisalimisha.” Kwa njia hiyo: “Tumaini la Papa linasalia kuwa lile lile linalorudiwa kila mara katika miaka ya hivi karibuni na hata hivyo  hivi karibuni lilirudiwa katika kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu kuzuka kwa vita kuwa: “Wakati ninapyaisha mapenzi yangu ya kina kwa watu wa Ukraine wanaoteswa na kuomba kwa ajili ya kila mtu, hasa kwa ajili ya waathiriwa wengi wasio na hatia, ninaomba kwamba kidogo huo wa ubinadamu upatikane ambao unaturuhusu kuweka mazingira ya suluhisho la kidiplomasia katika kutafuta amani ya haki na ya kudumu.”

Maelezo kuhusu kauli ya Papa kwenye mahojiano
10 March 2024, 09:58